Pages


Photobucket

Wednesday, October 17, 2012

ZANZIBAR NAKO HALI TETE,BAADHI YA MAJENGO YA OFISI ZA CCM YATEKETEA KWA MOTO


  Moja ya Ofisi ya CCM Zanzibar Ikiteketea kwa  moto

Taarifa kutoka mjini Zanzibar  zinasema kuwa hivi sasa Zanzibar kuna vurugu Kubwa wana uhamsho wanamtafuta Kiongozi wao aliyetekwa Jana usiku. Kwa hiyo Eneo la Darajani hapakaliki.

Habari zilizogaaa kila kona sasa hivi unguja kuwa Sheikh Farid wa Uamsho ametekwa na watu wasiojulikana na hadi sasa hajulikani yuko wapi.
Kwa mujibu wa Katibu wake, Abdallah Said Ally, amesema alikuwa na dereva wake maeneo ya Michenzani akitokea nyumbani kwake Mbuyuni, ndipo akakutana na gari moja ambalo dereva halifahamu na akashuka mwenyewe kwenye gari lake na kuingia katika hilo gari na kuanzia hapo hadi sasa hajulikani alipo.

Katibu huyo wa Uamsho na wenzake wamekuwa katika juhudi za kutuliza jazba za wafuasi wao na sasa wanawasiliana na polisi kujua alipo kiongozi wao.

Sheikh Farid 'amepotea' muda ule ule ambao inadaiwa mwenzake (Sheikh Ponda) alikamatwa (saa 4 usiku wa kuamkia leo jijini  Dar).

Hata hivyo, wananchi wa hapa Zanzibar wanasema polisi, UAMSHO na serikali wangesubiri wanafunzi wamalize mitihani ya Form 4 kabla ya wao kuanza malumbano yao!

Kutokana na Vurugu hizo Sehemu ya ofisi ya Chama Cha Mapinduzi imechowa moto na kwa kiasi kikubwa imeungua na hakuna aliyeripotiwa kuumia wala kupoteza maisha katika vurugu zinazoendelea sahivi huko zanzibar.
    
TASWIRA  HALISI YA VURUGU KUTOKA KISIWANI ZANZIBAR


No comments:

Post a Comment