Pages


Photobucket

Wednesday, October 24, 2012

NAPE NNAUYE AWA KIVUTIO MKUTANO MKUU WA UVCCM, DODOMA

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akicharaza gita zito la besi na bendi ya Vijana Jazz, wakati wa Mkutano Mkuu wa nane wa UVCCM kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere mkoani Dodoma.

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,
amenogesha Mkutano mkuu wa nane wa Umoja wa Vijana wa CCM, UVCCM
unaoendea mjini  Dodoma.

Licha ya viongozi wengi kushangiliwa wakati wa kuingia ukumbini,
nderemo na shamaramshamra zililipuka zaidi kutoka kwa wajumbe wa
Mkutano huo wakati Nape alipotangazwa kuwasili.

"Jembe, jembe, jembe", wajumbe walisikika wakilipuka na kumshangilia
baada ya Mkuu wa Umahasishaji na Chipukizi wa UVCCM, Esther Bulaya
alipotangaza kuwasili kwa Nape ukumbini.

Ukumbi ulilipuka zaidi Nape alipopanda jukwaani na kuliungurumisha
gita zito la besi, wakati Bendi ya Vijana Jazz ilipokuwa ikitumbuiza
wimbo maalum, baada ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuwasili ukumbini.

Viongozi wengine walioonyesha kuwakuna wajumbe wa mkutano huo wa
vijana ambao ni wa Uchaguzi Mkuu ni pamoja, na Mbunge wa Bumbuli
Januari Makamba, Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba na
Katibu wa NEC Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma.

Baada ya mkutano kufunguliwa na Rais Kikwete, uchaguzi uliendelea
ambapo leo, wanatarajiwa kupatika viongozi wapya wa UVCCM ngazi ya
Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
(NEC), Ujumbe wa Baraza Kuu UVCCM na wawakilishi kwenye jumuia
zingine.
Katika nafasi ya Uwenyekiti ushindani ulihamia kwa wagombea wawili
Msaraka Rashid Simai, Khamis Sadifa Juma baada ya mgombea mwingine
Abdallah Lulu Mshamu kujitoa wakati wa kujieleza kwa wajumbe ukumbini.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wamechuana Ally Salum Hapi, Paul Christian
Makonda Mboni Mohamed Mhita wakati nafasi zingine ni, Halmashauri Kuu
ya Taifa Viti sita (Bara) wagombea 40, Viti Vinne (Zanzibar) wagombea
22, Nafasi ya Baraza Kuu la Vijana Taifa Viti vitano Bara wagombea 39
na viti vitano Zanzibar wagombea 14,  Uwakilishi Wazazi Taifa na
Jumuia ya Wanawake Tanzania (UWT) wagombea 16 kila nafasi.

No comments:

Post a Comment