RAIS MWAI KIBAKI
Rais wa Kenya Mwai Kibaki, amekataa kuidhinisha mipango ya wabunge wa taifa hilo kujipatia kitita kikubwa cha pesa kama marupurupu ya kuhudumu kama wabunge.
Rais wa Kenya Mwai Kibaki, amekataa kuidhinisha mipango ya wabunge wa taifa hilo kujipatia kitita kikubwa cha pesa kama marupurupu ya kuhudumu kama wabunge.
Lakini bwana Kibaki amesema kuwa 
hatua hiyo inakiuka katiba na haiwezi kutekelezwa wakati ambapo walimu 
pamoja na madaktari nchini Kenya wamekuwa wakigoma kudai nyongeza ya 
mishahara. 
Waandamanaji waliojawa na ghadhabu nchini Kenya 
walijitokeza hapo jana kulaani hatua ya wabunge  hao kutaka kujilipa 
mamilioni ya pesa kama pesa za ziada wakati bunge litakapofunga vikao 
vyake kwa maandalizi ya uchaguzi mwaka ujao.
Waliwataja wabunge hao kama fisi wenye ulafi.
Wabunge wa Kenya ni baadhi ya wale wanaopokea 
mishahara mikubwa sana barani Afrika , wakipokea takriban dola elfu 
10,000 kama mshahara kila mwezi.
Malipo hayo ya ziada ya dola 110,000 kwa kila 
mmoja walitaka yalipwe wakati  watakapofunga vikao vyao kwa maandalizi 
ya uchaguzi mkuu mwaka 2013.
Wadadisi wanasema kuwa wananchi wangetozwa kodi zaidi ili kugharamia malipo hayo ya dola milioni 23.
Hatua hii imewakasirisha watu wengi, hasa 
ikizingatiwa kuwa inakuja baada tu ya migomo katika sekta ya umma ambapo
 madaktari, walimu na hata wahadhiri wa vyuo vikuu walisusia kazi 
wakidai nyongeza ya mishahara.
Mswaada huo ulipitishwa siku ya Alhamisi ikiwa sehemu ya mabadiliko yaliyofanyiwa mswaada wa fedha bungeni.
Mnamo mwezi Septemba, shule za umma zilifungwa 
kwa wiki tatu wakati walimu walipogoma wakidai nyongeza ya mishahara na 
huku madaktari nao wakitaka mazingira bora ya kazi.
***Chanzo cha habari ni BBC- Swahili**** 


No comments:
Post a Comment