Kiwanda cha silaha kilicholipuka Sudan
Kumetokea mlipuko mkubwa katika kampuni ya kutengeneza silaha katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum.
Mlipuko huo ulisababisha moto mkubwa na milipuko
zaidi ilifuatia wakati wazima moto walifika kujaribu kuudhibiti moto
huo, uliozuka kutoka kampuni hiyo ya Yarmouk .
Gaavana wa eneo hilo (Abdul Rahman Al-Khider
Rahman) amesema watu kadha wamepelekwa hospitalini baada ya kuvuta moshi
lakini hakuna aliyefariki.
Amesema kuwa mlipuko wa kwanza ulitokea katika
hifadhi ya silaha na bado chanzo chake kinachunguzwa. Vifaa vingi vya
kijeshi viko karibu na kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment