Pages


Photobucket

Saturday, May 25, 2013

HUYU NDO BINTI ALIYETOROKEA UINGEREZA AKIKWEPA KUTOMASWA NA MFALME MSWATI



Msichana mdogo ameomba hifadhi ya ukimbizi nchini Uingereza baada ya kukataa kwa dharau harakati za ndoa za wake wengi za Mfalme Mswati III wa Swaziland na kugoma kujiunga kwenye nyumba harimu ya wake 13.

Tintswalo Ngobeni, mwenye umri wa miaka 22, alitimkia Uingereza kutoka taifa hilo la kusini mwa Afrika akiwa na umri wa chini ya miaka 18 baada ya kuvuta hisia za mfalme huyo milionea, mtawala maarufu mkandamizaji kwa maisha yake ya anasa.


Ikiwa ni sehemu ya mila za Swazi, Mfalme Mswati III, mwenye umri wa miaka 45, anaruhusiwa kuchagua mke mpya kila mwaka.
 
Tintswalo, ambaye sasa anaishi mjini Birmingham, alikuwa na umri wa miaka 15 tu wakati Mfalme huyo alipofanya harakati zake baada kumuona kwenye jumba la kifalme la mke wake wa nne, LaNgangaza. Binti huyo alisema 'alitishika' pale alipogundua dhamira zake za ndoa.
Aliongeza: "Alianza kunipigia simu kwenye shule ya bweni. Aliniuliza kama ningetaka kuwa sehemu ya familia ya kifalme. Ilinibidi kukaa kimya kuhusu mashaka yangu lakini nilifahamu sikutaka kuolewa naye na kujitolea maisha yangu kwa mfalme huyo.
"Wake zake wamewekwa kwenye majumba yao, wakizingirwa na walinzi, na hakika hawawezi kwenda kokote isipokuwa tu mfalme akisema hivyo. Kitu pekee wanachofanya ni kwenda Marekani mara moja kwa mwaka, wakati mfalme huyo anapowapatia posho kwa ajili ya manunuzi."

Tintswalo alikuwa amelazimishwa kuachana na maisha ya starehe kwenye shule moja ya bweni huku shangazi yake, ambaye alikuwa mlezi wake mkuu, akisuka mipango ya kutorokea Uingereza kuungana na mama yake, ambaye alihamia mjini Birmingham miaka mitano kabla, akimtoroka mume wake mnyanyasaji.

"Sikuwa na jinsi," alisema. "Hakuna aliyewahi kumwangusha mfalme huyo au kuthubutu kumdharau, hivyo nikatoweka tu."

Tangu kuwasili nchini Uingereza, Tintswalo amekuwa sauti ya upinzani dhidi ya utawala kandamizi za Swazi, ambapo vyama vya upinzani vya siasa vimefungiwa na wanaharakati wamekuwa wakikamatwa mara kwa mara au kushambuliwa.

Hatahivyo, shughuli kuu za Tintswalo, ikiwamo maandamano ya kila wiki nje ya ubalozi wa Swazi mjini London akiwa na kikundi cha Swazi Vigil, zimesikika kwa mamlaka hizo nchini kwake na sasa anaamini yuko kwenye hatari kubwa zaidi kuliko ilivyowahi kutokea.

Alisema: "Hivi karibuni nilipata taarifa kwamba watu wametumwa kutoka Swaziland kuja kunikamata, jambo ambalo hakika linanitisha mno. Kama nikirejea, nitakamatwa au mbaya zaidi huku pale kuna watu ambao wanateseka, kupigwa au kuuawa kwa kujihusisha na siasa."
 
Tintswalo sasa anaishi katika mashaka ya kuweza kurejea nchini Swaziland, baada ya ombi lake la kwanza la hifadhi ya kisiasa nchini Uingereza mwaka 2007 kukataliwa mwaka 2011.

Mwezi uliopita, alikamatwa na kupelekwa kwenye kituo cha kushikilia wahamiaji baada ya miezi 18 ya kuripoti kila wiki katika mamlaka hizo.
 

Hatahivyo, baada ya shinikizo kutoka TUC na ofisi ya Mbunge wa Birmingham kupitia chama cha Labour, Roger Godsiff, Tintswalo aliachiwa na sasa amekata rufaa wizara ya Mambo ya Ndani.
 

Godsiff alisema juzi: "Tumefurahishwa mno wanasheria walifanikiwa sana katika kuwezesha kutazamwa upya kwa kesi ya Ngobeni."

Baba huyo wa watoto 27, Mfalme Mswati III alikuwa mgeni kwenye harusi ya William na Kate na pia kwenye sherehe za Miaka 50 ya Malkia wakati wa majira ya joto mwaka jana.

Mke wa sita wa mfalme huyo alitoroka kutoka kwenye jumba hilo harimu mwaka jana, akielezea miaka kadhaa ya 'machungu na udhalilishaji wa kimwili' uliofanywa na mume wake. 
 
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani alikataa kuzungumzia chochote.

DIAMOND ATIA AIBU YA MWAKA....KINGERZA CHAMUUMBUA TENA

KWANZA  NAANZA  KWA  KUMPONGEZA  SANA  DIAMOND maana  akiwa hajamaliza hata wiki mbili tangu atoke kwenye tour iliyofanikiwa ya Burundi na Congo, Diamond leo amesaini mkataba wa show nyingine kubwa ya kimataifa.

Kupitia Instagram, Diamond ameshare picha inayomuonesha akisaini mkataba wa show huku pembeni akiwepo mtu mwenye asili ya Asia ambaye huenda ndio promoter. 

Kilichowafanya  mashabiki wake  huko instagram  wavunjike  mbavu  ni Kingereza  alichotumia.....
"After I DONE did the Uk,Congo,Burundi…guess where next I’ll be headed.”...

Haijalishi  umekosea au upo  sahihi, ujumbe  umefika  kaka!!.  Waache  wacheke, wataacha  tu.

 Hata  hivyo, si vibaya pia  kutumia  lugha  yetu ya kiswahili  maana  ujumbe  hufika  vizuri  zaidi....Kingereza lugha ya  watu...ni ngumu..!!! 

WAASI WA M23 WATISHIA KUTUVAMIA MUDA WOWOTE....SERIKALI YA MKOA WA KAGERA YATOA TAHADHARI KWA WANANCHI

Serikali ya Mkoa wa Kagera imewatahadharisha wananchi wake kuepukana na wageni wasiowafahamu kwenye maeneo yao kutokana na tishio la kikosi chaM 23 cha nchini Congo DRC kinachotishia kuivamia Tanzania...
Kumekuwa na mapigano  makali  kati  ya waasi wa M23  na  vikosi vya serikali  nchini  Congo ambako jeshi letu lipo huko...
Waasi  hao  wametishia  kuivamia  Tanzania  muda  wowote  ili  kulipiza  kisasi.Miongoni mwa mipaka ambayo iko wazi  ni Kagera, na hii ndo sababu iliyopelekea  serikali ya Mkoa huo kutoa tahadhari kwa wananchi wake na watanzania kwa ujumla....

HATIMAYE DR. SLAA AKUBALIWA KUOANA NA MPENZI WAKE...





HATIMAYE Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imekatwa na aliyekuwa mume wa Josephine Mushumbusi( KWA  SASA  NI  MCHUMBA WA DR. SLAA) , Maimbo baada ya kuiona rufaa hiyo haina msingi wowote kisheria.

Hukumu hiyo ya rufaa ya  madai ya ndoa Na.32/2012 ilitolewa leo na Hakimu Aniseth Wambura ambapo alisema mahakama yake imefikia uamuzi huo wa kuitupa rufaa hiyo kwasababu haina mantiki ya kisheria.

Hakimu Wambura alisema mahakama yake imekubalina na hukumu iliyotolewa Aprili 2012 na Mahakama ya Mwanzo Sinza katika kesi ya madai talaka iliyokuwa imefunguliwa na Mushumbusi anayetetewa na wakili wa kujitegemea Philemon Mutakyamilwa  dhidi ya Maimbo ambapo mahakama hiyo ya chini ilitangaza kuwa hakukuwa na ndoa baina ya watu hao kwasababu Maimbo alikuwa ni mzinzi, simwaminifu katika ndoa yake na alikuwa akimtesa mkewe.

“Baada ya mahakama yangu kusikiliza hoja za mwomba rufaa na mjibu rufaa ,mahakama hii imefikia uamuzi wa kukubali hoja za Mushumbisi kuwa kwa tabia ile ya mbaya ya uzinzi na ukosefu wa uaminifu katika ndoa yake hapakuwepo na ndoa baina yao hivyo mahakama yake inatangaza kuwa hukumu ya mahakama ya Mwanzo Sinza ambayo iliivunja ndoa hiyo ilikuwa hukumu sahihi “alisema hakimu Wambura.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo wakili Mutakyamilwa alisema amefurahishwa na hukumu hiyo kwani mahakama imetenda haki  kwasababu kesi hiyo ya madai ya talaka ilikuwa na msukumo wa siasa chafu zilizokuwa na lengo chafu la kumchafulia jina mteja wake(Mshumbusi) ambaye kwa sasa ni mzazi mwenzie Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Wilbroad Slaa.
KWA  HIYO, KWA  SASA  DR. SLAA   NA  MPENZI  WAKE  W ANAWEZA  KUOANA..!!!

PASTA ATEMBEZWA UCHI HADI KANISANI KWAKE BAADA YA MKEWE KUMFUMANIA NA MWANAKWAYA LIVE

Mtumishi mmoja wa Mungu amejikuta akipata aibu ya mwaka si tu mbele za Mungu bali hata kwa mkewe pamoja na mashuhuda wengine baada ya mkewe kumfumania ‘live’ kitandani akifanya mapenzi na mwana kwaya wa kanisa lake huko Kisumu nchini Kenya.
 

Habari zilizoripotiwa na mtandao wa Kenyan-Post zinasema msichana huyo mweye miaka 23 amekuwa na mahusiano ya muda mrefu na pasta huyo kabla hawajabambwa.
 
Kisa hiki ni kama movie ambazo tumezoea kuziona zenye story line ambayo unaweza kutabiri mwisho wake.
 Kwa mujibu wa mtandao huo, ile ‘siku ya 40’ mke wa pasta huyo alikuwa anatarajia kusafiri kwenda nyumbani kwao kusalimia wazazi wake hivyo mumewe alimsindikiza mpaka kituo cha basi, lakini alionekana kuwa mtu mwenye haraka na kumwambia mkewe kuwa siku hiyo ana mkutano muhimu hivyo anapaswa kuwahi. Baada ya kumfikisha kituoni aligeuza gari kwa haraka na kuondoka.
Huku nyuma mke wa pasta kwa bahati mbaya (upande wa pasta) na bahati nzuri (upande wake) aligundua kuwa amesahau zawadi aliyokuwa amemnunulia mama yake mzazi ambaye ndio anaenda kumsalimia hivyo ikabidi airudie nyumbani kisha asafiri na basi litakalokuwa linafuata.
 
Alipofika nyumbani anapoishi na mumewe alishangaa kukuta mlango haujafungwa kwa nje na huku anakumbuka walipoondoka waliufunga hivyo akahisi huenda wamevamiwa mchana kweupe, alipojaribu kuusukuma ulikuwa umefungwa kwa ndani ndipo alipoomba msaada wa majirani wakavunja kitasa na kuingia ndani.
 
Mama huyo alipigwa na butwaa kwa kile alichokikuta ndani baada ya kumkuta msichana anayemfahamu kuwa kiongozi wa kwaya ya kanisani la mumewe wakiwa uchi wa mnyama katika kitanda chake na mumewe.
Maamuzi aliyochukua ni kuwavamia kitandani na kuzitupa nje kupitia dirishani nguo zao wote lakini kwa bahati mbaya msichana aliyemfumania alifanikiwa kukimbia na kumuacha pasta mwenyewe. 
 
Huwa wanasema hasira ni hasara na maamuzi ya hasira hugeuka majuto baadae, baada ya mmbaya wake kukimbia aliamua kumvuta mumewe (pasta) akisaidiwa na watu wengine  akiwa uchi wa mnyama na kumtembeza mbele ya umati wa watu mpaka katika kanisa analotoa huduma pasta huyo kwa lengo la kufichua mabaya yake.
 

AIBU: MUME WA MTU ANASWA NA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI GESTI


INAUMA sana! Wakati wazazi wakihenyeka na wakati mwingine kujinyima ili mabinti zao waweze kupata elimu bora itakayowasaidia maishani mwao wapo wapuuzi wanaokatisha jitihada hizo.

Mwanaume mmoja aitwaye Taliki Juma mkazi wa Temeke – Wailesi jijini Dar es Salaam ameingia  katika  dimbwi la AIBU baada ya kunaswa akiwa na mwanafunzi wa kidato cha pili wakifanya mchezo mchafu.

 

Mbaya zaidi, bila haya wala soni, Taliki alimwingiza binti huyo (jina na shule anayosoma vinahifadhiwa kwa sababu za kimaadili) katika chumba anachoishi na mwanamke anayedaiwa ni mke wake ambaye alikuwa safarini.


Chanzo chetu cha habari kilipiga simu chumba cha habari na kueleza juu ya tabia ya Taliki ya kwenda na denti huyo chumbani kwake tena akiwa kwenye sare za shule.

Kikao cha dharura kiliitishwa haraka baada ya sosi wetu kutoa maelekezo juu ya habari hiyo ambapo kwa muda huo na foleni za jiji la Dar usafiri uliopendekezwa ukawa ni pikipiki.

Haraka timu ya waandishi  wetu ilielekea eneo la tukio lakini kwa bahati mbaya walikwama. Taarifa iliyopatikana kutoka kwa mtoa habari wetu ni kwamba, muda mfupi kabla timu haijaingia eneo la tukio, Taliki alifanikiwa kukwepa mtego baada ya kumuondoa denti huyo.
 
Wikiendi iliyopita Mei 18, mwaka huu chanzo chetu kilekile kilipiga tena simu kwa mwandishi yuleyule na kueleza kuwa jamaa kwa mara nyingine amemwingiza yule denti chumbani kwake.

Timu A iliondoka na kwenda moja kwa moja hadi eneo la tukio na kuliweka chini ya uangalizi huku timu B ikielekea katika Kituo cha Polisi cha Wailesi na kuomba ushirikiano wao.
Timu ya maaskari wa kituo hicho wakiwa tayari kwa lolote, waliungana na waandishi wetu kwenda eneo la tukio.
Waandishi wetu, maaskari na wazee wachache wa mtaani hapo walivamia katika chumba hicho na kufanikiwa kumnasa laivu Taliki akiwa na denti huyo kama walivyozaliwa akimfanyisha mambo ya kikubwa muda ambao alitakiwa kuwa darasani.


Binti huyo ambaye alionekana kushtuka sana baada ya kukutwa chumbani hapo, alieleza kuwa amekuwa katika uhusiano na Taliki kwa muda mrefu baada ya kumrubuni kwa fedha na zawadi mbalimbali.
“Ni kweli huyu hapa ni mpenzi wangu, huwa ananipa pesa. Nyumbani kwetu ni Mwananyamala na nimetoka nyumbani nikienda tuisheni lakini Taliki aliniambia nije kwake.
 
“Naombeni mnisamehe jamani. Mama akijua atanipiga sana. Nisameheni tafadhali na ninaahidi mbele yenu kuwa nitaachana kabisa na huyu mbaba (Taliki),” alisema denti huyo.
 

Denti huyo alitoa namba ya simu ya mama yake mzazi ambapo alipigiwa na kufika eneo la tukio na kujionea jinsi mtoto wake anavyoharibiwa wakati yeye akiwa kwenye juhudi za kumtengenezea maisha. 

Mama wa binti huyo, hakuamini alichokiona na alijikuta akimwaga machozi muda wote, watu wazima wakapata kazi ya kumtuliza.
 
UPUUZI WA TALIKI
“Ni kweli nakubali huyu ni mpenzi wangu na nipo naye muda mrefu ila naombeni sana mnisamehe, kwa kweli ni shetani tu alinipitia (Mh! Huyu shetani anasingiziwa mengi sana).
 
“Ndugu zangu wakijua hili jambo watanitenga, naombeni muwe na roho ya huruma (utadhani na yeye ana huruma), maisha yangu yataharibika (sijui alikuwa anamtengenezea yule binti  wa watu maisha?).”
 
Utetezi wake haukusaidia na badala yake alifikishwa katika Kituo cha Polisi Wailesi na kufunguliwa mashitaka katika Jalada namba WS/RB/585/2013 – KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI.

 GPL

JACKLINE WOLPER NA BABY MADAHA WASHIKANA MASHATI WAKIGOMBANIANA NYUMBA YA KUPANGA


Sakata la wawili hao lilifika polisi na kubainika kuwa Madaha alilipa kodi kwa tapeli wakati Wolper alitoa fedha zake kwa mwenye nyumba hivyo kumfanya awe na haki ya kuhamia.
 

Akizungumza na mwandishi wetu, juzi jijini Dar es Salaam, Madaha alisema pamoja na kubainika kuwa alitapeliwa, mtu pekee ambaye angeweza kumsaidia kupata fedha zake (shilingi milioni tatu) ni Wolper lakini anamchenga.

“Ni kweli nimetapeliwa lakini Wolper kama msanii mwenzangu alikuwa na uwezo wa kunisaidia maana yeye anaishi pale lakini nimemwambia, ananipiga chenga. Sitaongea naye milele, hana utu kabisa. Milioni tatu ndugu yangu si pesa ndogo.”


KAULI  YA  WOLPER

Wolper alipotafutwa na kusomewa malalamiko ya Madaha alisema: “Naweza kusema Madaha hana akili, ni mpuuzi kwa sababu angekuja kwa busara nyumbani kwangu tungezungumza na baba mwenye nyumba tukajua namna ya kumsaidia.
“Lakini yeye kabla hajaomba ushirikiano kwangu, tayari naanza kusumbuliwa na magazeti kuwa eti nimemtapeli. 

Halafu hajawahi kunipigia simu bali alikuwa anawatuma watu wake kwangu. Kwa nini asingekuja mwenyewe?
 

“Ina maana yeye ni staa sana au? Huyu hana lolote anataka kupanda kwa kutumia jina langu,” alisema Wolper.

"NILIJIUNGA CHADEMA ILI NISAIDIE HARAKATI ZA UKOMBOZI WA TANZANIA NA SINA MPANGO WA KUGOMBE UBUNGE" ... PROFESA JAY

Mchawi wa rhymes, Profesa Jay amesema hakujiunga na CHADEMA ili mwaka 2015 awanie ubunge kama wengi wanavyodhani.




Rapper huyo wa ‘Machozi, Jacho na Damu’ ambaye jina lake halisi ni Joseph Haule, ameliambia gazeti la Mwananchi la leo kuwa amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ili kukisaidia chama katika changamoto za kuikomboa nchi.

“Kujiunga na siasa si dhambi na haina maana kwamba nina mpango wa kugombea jimbo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Sihitaji kugombea hata udiwani ila ni kwa dhumuni la kutaka kuongeza nguvu katika chama ili kuyafikia malengo,” ameliambia gazeti hilo.
 

Ameliambia kuwa yeye ni mfuasi wa Chadema tangu mwaka 2005 na amekuwa karibu na chama kwa nyakati nyingi lakini kwa sasa ameamua kuingia rasmi katika chama kama chachu katika kuongeza harakati kwa vijana.
 

“Nimeingia ili nisaidie hiki chama kuikomboa Tanzania kwani kwa muda mrefu niliokaa katika chama hiki nimegundua kuwa wamedhamiria kumkomboa msanii, kijana wa kawaida na wakubwa kwa wadogo hivyo nadhani nipo sahihi katika uamuzi wangu.”

BLA_EUCCQAEHZCc
“Natambua mimi ni mwanamuziki, sawa nina mashabiki wengi lakini haina maana kwamba sina haki ya kuchagua chama ninachoona mimi kinanifaa, lakini siwezi kusita kufanya kazi sehemu yoyote au wakati wowote chama kikinitaka nifanye kwa wakati husika,” alisema Profesa J

Tuesday, May 21, 2013

RAIS BARACK OBAMA KUTUA TANZANIA TAREHE 1 JUNE 2013



 Imeelezwa kuwa ujio wa Rais Barack Obama wa Marekani nchini, ni fursa nyingine kwa Tanzania kukuza uchumi na kuimarisha uwekezaji.
 Hata hivyo, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ni mchumi kitaaluma, amesema kuwa ujio wa Rais Obama unaweza kuleta neema hasa kama atakuwa ameambatana na wataalamu wa masuala ya maendeleo.
Hii itakuwa ziara ya pili ya Rais Obama katika Bara la Afrika.
Ziara yake ya kwanza aliifanya wakati wa awamu yake ya kwanza madarakani, wakati ziara ya safari hii ni kipindi chake cha lala salama.
Rais Obama alianza rasmi awamu yake ya kwanza kama Rais wa Taifa kubwa, Januari 20, 2009, wakati ng’we yake ya mwisho ilianza Januari 21, 2013.
Rais Obama anatarajiwa kufanya ziara hiyo mwishoni mwa Juni mwaka huu, ambapo Tanzania itakuwa miongoni mwa nchi za mwanzo za Afrika Mashariki kutembelewa na kiongozi huyo.
Ziara ya Rais Obama inafanyika baada ya ziara ya Rais Xi Jiping wa China aliyeitembelea Tanzania Machi 28, mwaka huu, ambapo Tanzania ilikuwa nchi yake ya kwanza kuitembelea kwa Afrika tangu achaguliwe kuwa rais, Machi 14, 2013.
Akizungumzia ziara hiyo tarajiwa, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (Cuf), Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ni mchumi, alisema amani, utulivu na uimara wa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi kwa kulinganisha na nchi nyingine za jirani, vimechangia kuwapo kwa ziara hiyo.
Profesa Lipumba alisema pia ugunduzi wa rasilimali za asili kama vile gesi, mafuta na madini ya urani ni sababu nyingine iliyomfanya Rais huyo kuja nchini.
Hivyo aliwashauri viongozi wa Serikali kujipanga kwa ajili ya kufungua mlango huo mwingine wa uchumi na uwekezaji.
Alisema pamoja na hali hiyo pia kuna mambo ambayo yanaweza kuchafua taswira ya nchi kama vile ubovu wa miundombinu ya barabara, msongamano wa magari barabarani na msongamano wa meli bandarini wakati zikisubiri kushusha mizigo.
Jumatano ya wiki hii, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry alitangaza mbele ya wajumbe wa Kamati ya Ushirikiano kati ya Marekani na Afrika, kwamba Rais Obama hivi karibuni atafanya ziara Afrika.
Ingawa Kerry hakutoa maelezo zaidi ya nchi gani za Afrika ambazo Rais Obama atazitembelea, lakini baadhi ya vyombo vya habari vya Nigeria vilieleza kiongozi huyo atafanya ziara Tanzania, Rwanda na Nigeria.
Kiongozi wa kwanza wa Afrika kukutana na Rais Obama tangu awe Rais wa Marekani, alikuwa Rais Jakaya Kikwete aliyekutana naye Mei 2009, Washington, Marekani.
Kwa nini ni Tanzania na Rwanda
“Kenya asingeweza kwenda kutokana na suala la Rais na Makamu wake kutuhumiwa kuhusika katika mauaji ya kimbari yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu 2007/2008, kwani msimamo wa Marekani ni kutaka wahusika wa vitendo vile wakamatwe na kufikishwa mahakamani. Hivyo kwake kuwatembelea watuhumiwa asingeeleweka,” alisema Profesa Lipumba.
Alibainisha kuwa Rwanda ina uhusiano wa karibu na Marekani na pengine suala la mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) litachukua nafasi.
Kulingana na taarifa za Ikulu ya Marekani, Rais Obama alikuwa amepanga muda wake mwingi wa awamu ya pili ya uongozi wake kujihusisha na masuala ya Afrika ( Chanzo: mwananchi)

Uthibitisho wa Habari hizi pia ni kutokakana na kutangazwa kwenye BBC NEWS WORLD zikithibitisha siku ya Rais wa Marekani, Barack Obama  kuja Tanzania itakuwa ni tarehe 1/06/2013
 

SPIKA WA BUNGE AAMURU KUFUTWA KWA HOTUBA YA SUGU ILIYOSABABISHA BUNGE LISITISHWE ASUBUHI




Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mh Anne Makinda, ameamuru kambi ya upinzani kuyaondoa maneno yote yaliyomo kuanzia ukurasa wa kwanza mpaka wa 14 katika hotuba rasmi ya Kambi ya upinzani iliyosmwa na mbunge wa Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi ‘Sugu,’ ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Mh. Makinda ametoa amri hiyo baada ya Kamati ya Kanuni ya Bunge kujadili hotuba hiyo na kubaini kuwa ina kauli za uchochezi; na kusema kuwa kuwa Bunge sio sehemu kugombanisha wananchi, hivyo maneno yote ya uchochezi hayaruhusiwi.
 
Katika hotuba hiyo, Mh. Mbilinyi aliishutumu serikali kuhusika na kuteka nyara waandishi wa habari, kauli iliyopelekea Spika Makinda kuahirisha Bunge.

Thursday, May 16, 2013

SUPER STAR LADY J DEE LEO AKANA UVUMI WA KUUSALITI UTANZANIA


 Staa wa bongo kupitia bongo fleva amekanusha uvumi kuwa yeye atahama nchi yake na hichi ndicho alicho kiandika kupitia ukurasa wake wa twitter 
 
Lady JayDee @JideJaydee

"Kuna muda pesa tu ndio inaongea sijui nihamie Kenya nikaombe uraia huko? Au Malawi labda, mtanifuata?"
 

''Hivi watu huwa hawajui kutofautisha masihara na ukweli eti? Sasa nihame nchi kwa kumuogopa nani? hahami mtu hapa''

KAJALA KUIGIZA FILAMU YA MAISHA YAKE HALISI SEGEREA, APONGEZWA NA KUPONDWA.


News is that actress Kajala Masanja anatarajia kucheza katika filamu ambayo itaelezea maisha yake halisi ya kesi yake iliyokuwa ikimkabili. filamu hiyo itaelezea tangu mwazo wa issue hilo, mahakamani, segerea mpaka anatoka baada ya Wema Sepetu kumtolea faini ya sh. millioni 13. Kajala mwenyewe amesema ni kweli na kwasasa story na script ndiyo vinafanyiwa kazi. Hata hivyo wadau wanaweza kuwa na hamu ya kuiona filamu hiyo kama kweli itafanikiwa kuonyesha mazingira halisi ya mahakamani na segerea kama ilivyokuwa kwa mwigizaji huyo kabla ya kuwa uraiani ikichukuliwa kwamba bado ni shida sana kupata location katika taasisi za serikali hasa huko segerea ambako Kajala mwenyewe aliwahi kusema kuna mambo ya kuhuzunisha sana.

 Kwasasa inadaiwa Kajala anafanya filamu ya Princess Sasha chini ya Wema Sepetu huku tayari baadhi ya watu wakisema Kajala ana haraka sana pengine ameburuzwa na watu kuhusu kucheza story ya kesi yake kwakuwa bado mumewe yupo jela hajatoka lakini tayari yeye amepanga yake huku uraiani. Shabiki mmoja amesema " i think Kajala bado hajashauriwa vizuri kwa time hii kucheza maisha yake halisi hata miezi 2 bado kuisha". mashabiki wake wengine wamesema ni poa tu apige kazi " Kajala Nakuaminia Pamoja Sana Kazi Njema" amesema shabiki

MOVIE ALIYOFANYA MAMA KANUMBA KUTOKA KESHO MITAANI, HAWA NDO WAHUSIKA WAKUU

fffffffffffffffffffffffffffffff
Movie titled “Without Daddy” ambayo imepata kick kutokana na Mama Kanumba kuwa ndani yake, kesho itakuwa mitaani. Watu wengi wana hamu kubwa ya kuona jinsi gani mama Kanumba anauwezo kiasi gani kwenye ishu za kuigiza. Basi usikose kuikamata copy yako kesho na uangalie jinsi gani mama Kanumba kafanya mambo humu ndani. Kweli alimpa kipaji mwanae au ni vingine?

HATIMAE NEY WA MITEGO AZUNGUMZIA ISHU YA NIKI MBISHI KUTOA WIMBO UNAOITWA NEY WA MITEGO, SOMA HAPA ALICHOKISEMA

clip_image003 

Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya Ney Wamitego amesema Nikki Mbishi na wasanii wengi wachanga huwa wanajaribu kuwa-diss wasanii wakubwa kwa lengo la kupata jina.
Ney alizungumza hayo pale nilipotaka kujua kutoka kwake juu ya kitendo cha msanii Nikki Mbishi kutengeneza wimbo unaoitwa Ney Wamitego, wimbo ambao unaonekana moja kwa moja unamzungumzia Ney Wamitego kama mwanamke au mwanaume siyo.
Mwanzoni mwa mazungumzo yangu nilitaka kujua kutoka kwa Ney, anachukuliaje kitendo cha msanii huyo kuandika wimbo unaomzungumzia yeye, Ney alikataa kuzugumza hilo huku akisema "Yaani kaka mimi nikiongea kitu tu mimi nampa kick ile anayotaka yule dogo, mi sitakiwi kuongea kitu, yaani hiki ndio kitu ambacho watu wa karibu wamekuja wameniambia this time huyu amefanya hiki kwa sababu ya hiki, so dont talk anything"

HUYU NDIO MBUNGE KUTOKA KENYA ANAYEPANGA KUWAFUNGULIA MASHTAKA WAANDAMANAJI KWA KUANDIKA JINA LAKE KATIKA NGURUWE

Leader of Majority Aden Duale is now planning to sue organizers of Tuesday’€™s anti-MPs protest who symbolically used pigs that feasted on blood at the gate of Parliament buildings.
Duale is irked that the activists branded one of the pigs with his name and that of fellow legislators Jakoyo Midiwo and Mithika Linturi.
Pig.png
The pig with the legislators' names
The MP, who is also the Garissa Township legislator, is a devout Muslim whose religion forbids the association with pigs or swine that is considered unholy. I am planning to sue these fellows who branded me a pig, this is a big issue in my constituency right now,” he said in parliament.
Duale says that although the activists reserve their right to picket, it is unacceptable to tarnish his name as a practicing Muslim by labeling his name on a pig feasting on blood.
"This is an insult and an affront to my religious liberty by associating me with an animal that my religion prohibits," he said

MASTER JAY AFUNGUKA KUA TUZO ZA KILIMANJARO MUSIC AWARDS ZINALENGO LA KUDHALILISHA, SOMA ZAIDI ALICHOKISEMA



MTAYARISHAJI nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini, Joachim Kimario 'Master Jay' amesema amekosa imani na Tuzo za Kilimanjaro Music, kwa kuwa zinalengo la kuwadhalilisha baadhi ya wasanii.
Master jay amekosa imani kumetokana na Kamati ya Kilimanjaro Academia ambayo imepewajukumu la kuchagua wasanii kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho kukosa sifa.
Akizungumza Dar es Salaam juzi, Master Jay alisema tatizo linaanzia kwenye kamati hiyo kuchagua wasanii waliokosa sifa na vigezo, huku ikiwa haiko wazi kwa wadau pamoja na wasanii ambao ni washiriki wa tuzo hizo.
Alisema watu waliochaguliwa kwenye kamati hiyo, wamekosa uelewa wa muziki na ndiyo maana wanachagua baadhi ya wasanii waliokosa ubora na kusababisha kupoteza imani ya tuzo hizo kwa jamii nzima.
Mtayarishaji huyo alisema ndiyo maana baadhi ya wasanii wanajitoa kwenye kinyang'anyiro hicho kwa kuogopa kujidhalilika.
Sijui ni akina nani wanaounda kamati hiyo kwani imepoteza sifa na ndipo tatizo linapoanzia hapo kila mwaka, kukosa uelewa kwenye kamati hiyo na kutokuwa na uwazi kunachangia malalamiko ya kila siku kwa baadhi ya wadau wa muziki.
"Baadhi ya wasanii wanalalamika sana kuhusu tuzo hizi na ndiyo maana wengi wanajitoa, si kwamba wanajitoa kwa kuogopa kushindana hapana bali kudhailika kwani hizi tuzo sasa zinadhalilisha baadhi ya wasanii," alisema Master Jay
Hata hivyo aliwapongeza kwa kuongeza vipengele vingine kwenye tuzo hizo, ambapo mwaka jana kulikuwa na vipengere 29 na sasa vimeongezwa na kuwa 32.
"Kila mwaka wanapiga hatua 10 mbele na kurudi hatua 30 nyuma, hali ambayo inaonesha hakuna maendeleo yoyote kwenye upande wa tuzo hizo, hivyo wanahitaji marekebisho ili kuwe na usawa na kurudisha imani ya tuzo hizo kwa wasanii," alisema Master Jay.
Kwa upande wake Mratibu wa tuzo hizo kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Angelo Luhala alisema tatizo lipo kwa waandaaji ambao ni Kampuni Bia Tanzania (TBL) kushindwa kutoa elimu ya kutosha kwa wadau wote wa muziki nchini.
Alisema TBL inatakiwa kuelimisha umma kujua kazi ya Kilimanjaro Academia, inavyofanya kazi pamoja na mchakato mzima wa tuzo hizo zinavyokwenda, ili kuepuka ulalamikaji unaojitokeza kwa baadhi ya wadau wa muziki.
"Elimu ikitolewa kwa washiriki pamoja na wadau wa muziki, imani itarudi kwenye tuzo hizo na watajua mchakato mzima unavyofanyika hivyo uwazi wa jambo hilii ndiyo utapunguza malalamiko katika tuzo hizo," alisma Luhala.

HABARI NJEMA KWA WATUMIAJI WA BBM , IPHONE ,NA ANDROID


Blackberry wametoa taarifa kwamba wanampango wa kuifanya BBM kutumika katika simu za android na iphone.
Andrew Bocking, Executive Vice President of Software Product Management & Ecosystem at BlackBerry alisema kwamba
“Wateja wa blackberry wamekuwa wakitaka BBM iwepo pia kwenye Android na iOS ya iPHONE. Aliendelea pia kwa kusema BBM kwa sasa ina watumiaji 60 million.
Whatsapp ina watumiaji 160 million, nadhani hapo utaona umuhimu wa kuanzisha BBM kwenye Android na Iphone.”
Lakini watu wamekuwa wakijiuliza maswali endapo BBM itakuwa inapatikana kwenye Android na Iphone sasa kutakuwa na umuhimu gani wa kuwa na Blackberry?..

Home » burudani » WASANII WAFAFANUA AINA ZA RUSWA KWENYE MUZIKI, ZIFAHAMU HAPA WASANII WAFAFANUA AINA ZA RUSWA KWENYE MUZIKI, ZIFAHAMU HAPA

BAADHI ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya wafafanua aina za rushwa zinazotokea katika tasnia ya muziki ambazo zinasababisha kudidimiza muziki pamoja na vipaji vya wasanii.

Rushwa hizo ambazo zinatolewa na baadhi ya wasanii kwa baadhi ya vyombo vya habari kwa ajili ya kupiga muziki wa msanii hata kama hauna sifa,imezidi kuchukua sura mpya kwa kuhusisha baadhi ya mashabiki kwa ajili ya kuomba nyimbo katika radio.

Akifafanua aina ya rushwa hizo jijini Dar es Salaam Hugoline Martin 'Dj Choka' ambaye pia ni mmiliki wa mtandao wa Bongo Star alisema, kuna aina mbili za rushwa ambapo moja ilikuwa imezoeleka kwa wasanii kutoa hela kwa baadhi ya watangazaji wa redio ili kuwezesha nyimbo zao kupigwa kwenye vipindi ambapo rushwa hii imezoeleka kwa baadhi ya wasanii walio wengi nchini.

Kutokana na hali hiyo alisema muziki wa bongo fleva unakuwa kwa kusikilizwa kwa wingi kwenye baadhi ya vyombo vya habari huku ukiwa unakosa sifa ya ubunifu hali inayochangia kufanana kwa baadhi ya nyimbo kuanzia melody hadi mahudhuhi ya nyimbo.

Alisema kuwa rushwa ya aina ya pili  ni ile ya mashabiki ambao wanapewa hela na baadhi ya wasanii kwa ajili ya kuomba nyimbo redioni hali ambayo inaonyesha msanii fulani nyimbo yake kuombwa mara kwa mara hata kama haina sifa na imekosa ubunifu.

"Kuna rushwa nyingi sana kwenye muziki sasa kuna hii mpya ya baadhi ya wasanii kutoa hela kwa mashabiki wao ili kuomba nyimbo kwenye redio kwahiyo utaona nyimbo inaombwa sana hata kama haina sifa hii inasababisha kuushusha muziki wetu " alisema Choka

Akielezea kwa upande wake jinsi anavyofanya kazi na wasanii hao wa muziki wa bongo fleva alisema, ameweka vigezo kwa wasanii hivyo haweki nyimbo ambayo haina vigezo kwenye mtandao wake.

"Nimeshakataa kupigiwa simu na wasanii kuniomba niweke nyimbo yake kwenye mtandao wangu na mimi sipokei hela teyari wanafahamu hilo hivyo muziki ninaouweka kwenye blog ni ule wenye sifa na vigezo tu na siyo kwa ajili ya hela " alisema Choka

Kwa upande wake msanii wa bongo fleva kutoka kundi la TMK wanaume Amani Temba anayejulikana kwa jina la  'Mheshimiwa Temba' amesema kunatofauti kwa upande wa muziki kwa kipindi hiki na kipindi cha zamani ambapo hapo mwanzo muziki ulikuwa unasikika kwa nguvu ya prodjuza pamoja na msanii mwenyewe.

Alisema rushwa imejaa kwenye baadhi ya vyombo vya habari ambapo msanii nyimbo yake haipigwi mpaka atoe hela sababu inayosababisha kuwa na nyimbo nyingi kusikika redioni huku zikikosa sifa ya kuwa nyimbo bora .

HIVI NDIVYO CHAZ BABA ALIVYOMVISHA PETE MCHUMBA’KE JUKWAANI, STORI NA PICHA SOMA HAPA

PREZIDAA wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba,’ juzikati aliendeleza harakati za maandalizi ya ndoa kwa mashabiki wake baada ya kumvisha pete jukwaani mchumba’ke, Rehema Sospeter.

Charles Gabriel ‘Chaz Baba,’ akimvisha pete mchumba’ke, Rehema Sospeter.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na Amani lilijiri Mei 11, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama, Dar, wakati bendi yake ilipokuwa ikitambulisha albam mpya, Risasi Kidole.
Akizungumza na paparazi wetu mapema wiki hii, Chaz Baba alisema ameamua kuonesha uamuzi wake huo kuanzia kwa mashabiki wake waliofika ukumbini na kwa wale wasiofika kwa sababu wengi wao walikuwa hawamuamini.
“Nilifanya vile kukata vilimilimi ‘coz’ tangu nimegawa kadi za mchango wa harusi, kumekuwa na maswali mengi ambayo yanaashiria wengi hawaamini uamuzi wangu,” alisema Chaz.

POLISI 7 WATIWA MBARONI KWA KOSA LA " KUWATIA VIJITI MATAKONI " WATUHUMIWA NA KUSABABISHA VIFO

POLISI saba kutoka wilayani Kasulu, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, iliyoanza kikao chake mjini Kigoma leo na kusomewa mashitaka ya kuua kwa kukusudia. 
Mbele ya Jaji Sam Rumanyika, askari Polisi hao walidaiwa kuwa Agosti 6, 2011 walimpiga na kumuua kwa makusudi Festo Stephano, mkulima na mkazi wa Kijiji cha Rungwe mpya wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Waliopandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka yao ni pamoja na Baraka Hongdi, Koplo Mawazo, Koplo Swahib, Koplo Charles, Koplo Shamsi, Koplo Jerry na Koplo Amrani ambao kwa pamoja walikana mashitaka.
Baada ya kukana mashitaka, kesi hiyo ilianza kusikilizwa kwa mashahidi wa upande wa Jamhuri kuanza kutoa ushahidi wao, ambapo shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, Masumbuko Stephano, aliieleza Mahakama kwamba askari hao walikusudia kufanya mauaji hayo.
Masumbuko aliieleza Mahakama kwamba siku ya tukio, alikamatwa pamoja na marehemu na mgambo wa kijiji, na kuwekwa katika mahabusu ndogo katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata.
Alidai baada ya kufika, askari hao walianza kuwapiga kwa kutumia vitako vya bunduki, fimbo na chupa za bia, hali iliyosababisha wapatwe na maumivu makali.
Shahidi huyo alidai kuwa baada ya kupigwa na kukaribia kupoteza fahamu, polisi hao waliwavua nguo, wakawafunika na turubai ndani ya gari ambapo baadaye walinunua magunia ya mkaa na kuwakandamiza na magunia hayo.
Shahidi wa pili katika kesi hiyo, Andrea Sama, alidai kwamba askari hao walikusudia kufanya mauaji siku hiyo, kwani licha ya kutoa kipigo pia waliwavua nguo na kuwaingiza miti kwenye sehemu zao za haja kubwa.
“Mheshimiwa Jaji kwa kweli nilishuhudia vitendo vya askari hao kwa macho yangu, na nilishindwa kuamini kama jambo hilo linafanyika kwenye ardhi ya Tanzania au tuko nchi nyingine, maana unyama uliofanywa na askari polisi hao huwezi kudhani kama ni walinzi wa amani katika nchi hii,” alidai Sama.
Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa mfululizo hadi kutolewa hukumu, ambapo mwanasheria mwandamizi wa Serikali, Juvelin Rugaihuruza, alidai kuwa upande wa Jamhuri ambao ndiyo mlalamikaji, unatarajia kuwa na mashahidi 12 na vielelezo viwili.
Washitakiwa hao wanatetewa na Mwanasheria, Method Kabuguzi, kutoka Kampuni ya Uwakili ya Kigoma Law Chamber and Advocate ya mjini Kigoma.

Mgomo wa wafanyakazi 'wanukia' TRL

Chama cha Wafanyakazi wa Reli nchini  (Trawu),  kimeitaka Serikali kuongeza kiwango cha mishahara kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), vinginevyo kitaisimamisha treni ya abiria maarufu kama treni ya Mwekyembe. Akizungumza kwenye mkutano na wafanyakazi wa TRL jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Trawu Taifa, Erasto Kihwele, alisema kuwa wafanyakazi wamechoshwa na mishahara midogo wanayolipwa kwa miaka 15 sasa bila ya nyongeza.

Kiwhele alisema kuwa ni miaka 15 sasa toka Serikali ilipopandisha mishahara kwa wafanyakazi wa shirika hilo kutoka Sh. 50,000 mpaka 205,000 wakati gharama za maisha zimepanda huku wafanyakazi wa kada nyingine wakiongozewa mishahara kila wakati.
Aliongeza kuwa uongozi wa Trawu umeamua kwenda Dodoma kwa lengo la kuonana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ili kuzungumza naye kuhusu mustakabali wa nyongeza ya mishahara ya wafanyakzi wa kampuni hiyo.
“Kwa kweli safari hii tumeamua endapo hawatatupandishia nyongeza ya mishahara kwa asilimia mia moja tutaweka vitendea kazi chini na kuanza mgomo wa nchi nzima ili kuishinikiza Serikali,” alisema.
Alisema wameazimia kwenda Dodoma kuonana na Pinda baada ya kuona Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe na Naibu wake kushindwa kutatua matatizo yao.

DR. SLAA AMKIMBIA NAPE NNAUYE KATIKA OFISI ZA ITV

Katika tukio lisilo la kawaida ambapo kituo cha Matangazo cha ITV kiliandaa mjadala wa kujadili hali ya kisiasa nchini na masuala mbalimbali ya kitaifa ambapo kwa busara za watendaji wa ITV waliwaalika wasemaji wakuu wa mjadala huo kuwa Viongozi waandamizi wa Vyama vya Siasa wakianza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahaman Kinana naKatibu Mkuu wa CDM Ndugu Slaa.
Kutokana na hudhuri wa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana ambapo amesafiri kuelekea Dodoma kwenda kuhudhuria kikao cha kamati kuu jana na kubanwa na majukumu mengine muhimu ya kichama na kitaifa, alimuagiza Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM,ndugu Nape Nnauye kumuwakilisha katika mjadala huo wa viongozi wa vyama vya siasa katika kujadili hali ya kisiasa na mustakabali wan chi yetu.
Baada ya kufika katika Ofisi za ITV zilizopo mikocheni asubuhi ya Leo, Nape pamoja na Slaa walikutana na Nape kueleza kuwa atamuwakilisha Katibu Mkuu wake katika mazungumzo hayo ambapo baada ya kusikia kauli hiyo, Dr Slaa alianza kuhamaki na kudai kuwa hawezi kuongea na Nape kwa sababu anamtaja vibaya kwenye mikutano yake.
Hata busara zilipotumika za kumsihi apungumze munkari na kumtaka kuangalia umuhimu wa mazungumzo hayo na kipindi hicho kwa watanzania, bado Slaa aligoma na kuondoka katika ofisi za ITV.
Baada ya tahamaki hiyo, mijadala ya pembeni ya mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa kimsingi Slaa anamuogopa Nape katika mijadala ya kisiasa, nahii ni kutokana na uwezo wa Nape katika kujenga hoja na kuzilinda na kuzitetea hoja hizo...
Tukio hilo linadhihirisha kukosa uvumilivu wa kisiasa (lack of political tolerance) ambako viongozi wa CDM hasa Slaa wanao..... Hii ni kwa sababu Nape alimtaka aeleze ni kusemwa vibaya kupi ambako yeye Slaa anakumaanisha na akashindwa kubainisha.....
Hali hiyo pia imeonesha taswira ya political immaturity kuwa viongozi wa aina hii hawajakomaa ...
Pia, tukio hilo linaweka wazi kuwa CDM hawako tayari kuyazungumzia ana kwa ana matatizo yaliyotokana na Siasa mbovu za matusi....
Tabia hii ya kukwepa kuyashughulikia makosa ya kisiasa kutalileta Taifa letu madhara makubwa sana. ...kukataa kulikubali tatizo tulilonao la siasa mbofu zenye kuhamasisha chuki, utengano, udini, ukabila na hata kuendesha matukio ya kudhuru watu na mauaji ni makosa.

Skylight Band yazidi kukusanya maelfu ya mashabiki ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.

Binti mwenye kipaji cha aina yake Mary Lukas akiongoza waimbaji wenzake kutoa burudani Ijumaa iliyopita kwa mashabiki wa Skylight Band katika kiwanja chao cha nyumbani Thai Village Masaki jijini Dar.
Wapenzi wa Skylight Band na staili ya aina yake baada ya kuamua kutinga ukumbi na Vest hii ikimaanisha hawataki kusikia joto wakati wa kusakata muziki wa Band hiyo inayobamba nchini Tanzania.
Uzao wa BSS Mary Lukas akifanya yake jukwaani, Ewe Mtanzania Mary Lukas anaomba kura yako amechaguliwa kushiriki tuzo za Kilimanjaro Music Awards katika Category ya Mwimbaji Bora wa kike wa Band…Mpigie kura andika AM4 tuma kwenda namba 15345.
Watu wa ukweli wenye mapenzi ya kweli na Skylight Band…Wewe Je? Njoo Ijumaa hii ujionee vipaji.
Sam Mapenzi wa Skylight Band akivuta hisia kali wakati akitoa burudani kwa wapenzi wa Band hiyo.
Vijana wa Skylight Band wakimwimbia nyimbo ya Happy Birthday mmoja wa shabiki wa band hiyo aliyefahamika kwa jina la PAPITO, Ijumaa iliyopita ilikuwa ni kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.
Shabiki wa Skylight Band PAPITO akikata cake yake mbele ya jukwaa tayari kuwalisha wanamuziki wa band hiyo.
Birthday Boy PAPITO akimlisha cake mmoja wa marafiki zake.
PAPITO akimlisha cake Sam Mapenzi wa Skylight Band aliyewakilisha kikosi kizima cha Band hiyo. Mdau na wewe unakaribishwa kusheherekea Birthday yako pamoja na Skylight Band Ijumaa hii.
Rappa Joniko Flower akitoa burudani kwa wapenzi wa Skylight Band… Joniko ni miongoni mwa waimbaji bora wa kiume wa band aliyechaguliwa kushiriki tuzo za Kilimanjaro Music Awards 2013 anaomba kura yako wewe Mtanzania andika BG4 au AX3 tuma kwenda namba 15345.
Mwanamuziki mkongwe aliyewahi kuwa Jaji wa shindano la Bongo Star Search Mzee John Kitime akichukua matukio ya kumbukumbu huku akionyesha furaha ya aina yake kuona vipaji vya wanamuziki wa Skylight Band husuani Mary Lukas mshiriki wa BSS.
Mashabiki waliotia fora Ijumaa iliyopita baada kuja ukumbini hapo na Vest maalum kwa kusakata Sebene la Skylight Band ili wasisikie joto.
Aneth Kushaba AK 47 akitoa burudani kwa wapenzi wa Skylight Band huku akisindikizwa na Sony Masamba pamoja na Mary Lukas.
Aneth naye ni miongoni Waimbaji bora wa kike wa Band wanaowania Tuzo za Kilimanjaro Music Awards 2013 naye yeye pia anaomba kura wewe Mtanzani mpigie sasa kwa kuandika AM 1 tuma kwenda namba 15345.
Muziki wa Carolina unapokelea inakuwa hivi kwa fans wa Skylight Band.
Sam Mapenzi akionyesha ufundi kwa mashabiki wa band hiyo huku nao wakimuiga miondoko yake.
Kikosi kazi cha Skylight Band kikitawala Jukwaa na manjonjo ya aina yake.
Mashabiki walipagawaje na Sebene la Skylight Band.
Hapana chezea Skylight Band wewe….ni balaaa. Vibonge wepesi wakijimwaga na sebene.
Uliwadia ule muda wa Skylight Band kutambulisha nyimbo yao mpya ya mduara inayotambulika kama”Umechana Mbeleko”.
Mashabiki wakizungusha nyonga wakati wa kucheza mduara.
Hapo sasa wa mbele aende mbele wa nyuma arudi nyuma….
Mashabiki wakionekana kuchizika na wimbo huo mpya wa mduara wa band hiyo na kupiga makelele urudiwe tena na tena….Njoo Ijumaa hii uonje ladha yake.
Mrembo wa ukweli katika pozi matata mbele ya camera yetu.
Kadri siku zinavyokwenda Skylight Band inazidi kuongeza namba ya mashabiki wa band hiyo kwa kasi ya ajabu, baadhi yao ni hawa hapa.
Fans wapya wa Skylight Band wakishow love.
Picha juu na chini ni William Malecela wa Blog ya Jamii a.k.a LE MUTUZ akishow some love na Mabebsss wa ukweli.