Uhaba wa mafuta ya petroli na dizeli ambao umeendelea kuukumba mji wa Iringa kwa zaidi ya siku tano sasa, umeendelea kuwatesa wananchi wa kada mbalimbali ambapo jana, Mbunge wa jimbo la Wawi katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed (CUF) ameonja keor hiyo baada ya kuingia mjini Iringa na kujikuta akisota kwa zaidi ya saa nne katika foleni ya kusubiri kununua mafuta katika kituo cha kimoja wapo kilichokuwa kikiuza mafuta katika eneo la Ipogolo.
Mbunge Hamad alikuwa safarini kutokea mkoani Morogoro akielekea Mafinga wilaya ya Mufindi. Mbunge huyo amesema, "serikali inapaswa kuangalia uwezekano wa kutatua tatizo hilo la uhaba wa mafuta hapa nchini vinginevyo uchumi wa nchi utaendelea kuyumba zaidi"
Amesema kuwa kitendo cha wananchi kushinda katika foleni kwa saa zaidi ya sita wakisubiri kununua mafuta katika kituo hicho ni sawa na wananchi hao kupoteza muda wa kuzalisha, hivyo Serikali iliyopo madarakani inapaswa kushughulikia tatizo hilo ambalo linasababishwa na waagizaji wakubwa wa mafuta hapa nchini.
Mbunge huyo alisema alifika katika foleni hiyo majira ya saa 8 mchana na kufanikiwa kununua mafuta saa 12 jioni.
Mbali ya uhaba huo wa mafuta, uchunguzi uliofanywa na Francis Godwin (kutoka francisgodwinblog ) umebaini kuwa baadhi ya vijana walikuwa wakishirikiana na wafanyakazi wa vituo hivyo vya mafuta kwa kununua mafuta na kujaza katika mapipa na kupakia katika magari na kwenda kuyauza kwa bei kubwa zaidi mjini Iringa.
No comments:
Post a Comment