WAZIRI MKUU WA TANZANIA MIZENGO PINDA
Waziri Mkuu wa Tanzania,Mh Mizengo Pinda Akizungumza na Mtangazaji wa shirika la utangazaji BBC Bw. Salim Kikeke jana (18/10/2012) katika vipindi vyao vinavyorushwa kila siku za jumatatu-ijumaa kuanzia saa 3:00 usiku kupitia kituo cha Television ya Star Tv, Kikeke alitaka kufahamu Kwanini nchi kama Tanzania haifanyi vizuri katika michezo na badala yake kuwa wasindikizaji .
Akijibu swali hilo Mh Mizengo pinda alisema:-
"Lazima
tufanye jitihada kubwa kwanza kuahinisha watu wenye vipaji
hivi mapema tangu wanapokuwa kwenye shule hususani shule za msingi na sekondari na kuwajenga ,
Tangu zamani tulikuwa na
utaratibu huo ingawa hapa katikati ndio tukapiga marufuku mambo ya michezo mashuleni n.k.Nadhani hili ndilo lililo tuhathiri , Eneo ambalo
tulikuwa tunalichukulia kama
chachu likawa tena halipo, kwa hiyo tukawa tunangoja mpaka
itokee bahati nasibu kitu ambacho hakiwezekani.
Ile hali ya kutoruhusu hali hii kuendelea ,kwakweli tulivuruga sana kitu ambacho
kimetugharimu sana ,sasa tumeanza ikiwa ni pamoja na kuruhusu michezo mashuleni na michezo yote.
Na sasa tunayo mashindano kila mwaka ikiwa sasa ni kujaribu kuona ni nani wanaoweza na
wenye vipaji
wakiwa wadogo ili tuweze
kuwaendeleza kama tulivyo kuwa tuna fanya tangu zamani."
No comments:
Post a Comment