Muamar Gaddafi
Mwaka mmoja baada ya kukamatwa na kuuwa kwa kiongozi
wa zamani wa Libya, Muammar Gaddafi tarehe 20 mwezi Oktoba mwaka 2011,
familia yake iko wapi?
Watoto watatu wa Gaddafi waliuawa wakati wa
harakati za mapinduzi akiwamo aliyekuwa mshauri wake wa usalama wa
kitaifa Mutassim Gaddafi, aliyefariki mikononi mwa waasi siku moja na
ba
Jamaa za Gaddafi wanaosalia
wamekumbwa na hali tata tangu kifo cha Rais huyo mwezi Oktoba, huku
mjane wake akitafuta hifadhi katika nchi jirani ya Algeria, mwanawe na
aliyeonekana kama mrithi wa wake Saif al-Islam yuko gerezani nchini
Libya akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake kuhusu uhalifu wa kivita.
Safiya Farkash, mama wa watoto wanane wa Gaddafi amekuwa akiishi nchini Ageria alikopewa hifadhi kwa sababu za kibinadamu.
Pamoja na wanawe Ayesha na mwanawe wa kambo
kutoka kwa mke wa kwanza wa Gaddafi, waliingia nchini Algeria wakati
waasi walipoudhibiti mji mkuu Tripoli.
Amepewa hifadhi nchini humo na kuwekewa vikwazo na serikali vya kutotoa matamshi yoyote ya kisiasa wala kuingilia mambo ya Libya
Muhammad Gaddafi (Mwanawe)
Ikiwa mambo yangekwenda vinginevyo Muhammad
angehudhuria michezo ya Olimpiki 2012 kama mkuu wa kamati ya michezo
hiyo nchini Libya.
Badala yake, Muhammad mwanawe wa kwanza Gaddafi,
amekuwa nchini Algeria kwa mwaka mmoja sasa tangu kukimbilia huko
wakati waasi walipovamia mji wa Tripoli.
Ni mtoto wa mke wa kwanza wa Gaddafi, Fathia,
pia alikuwa mwenyekiti wa kampuni ya taifa mawasliano ya simu za mkononi
nchni Libya.
Hatakikani na mahakama ya ICC na hakuhusika pakubwa na kujaribu kuzima harakati za mapinduzi dhidi ya babake mwaka jana.
Saif al-Islam Gaddafi (Mwanawe Gaddafi)
Alionekana na wengi kama ,mrithi wa babake,
alikamatwa mwezi mmoja baada ya kifo cha babake, na amekuwa akizuiliwa
mjini Zintan tangu hapo.
Alihitimu kutoka chuo cha mafunzo ya uchumi
mjini London, na amekuwa sababu ya mvutano kati ya mahakama ya kimataifa
ya ICC ambako anakabiliwa na tuhumza za uhalifu wa kivita na maafisa wa
sheria nchini Libya ambao wanasisitiza kuwa lazima kesi yake iendeshwe
nchini humo.
Idara ya sheria nchini Libaya kwa sasa
inaonekana kushinda katika mvutano huo, lakini hakuna tarehe rasmi ya
kusikilizwa kwa kesi yake, inaarifiwa kuwa jela ya kifahari ikiwa na
uwanja wa mpira wa vikapuni na mpishi wake binafsi vimeandaliwa kwa Saif
mjini Tripoli
Saadi Gaddafi (Mwanawe Gaddafi)
Saadi Gaddafi, aliyekuwa mkuu wa shrikisho la
soka nchini Libya pamoja na kuongoza vikosi maalum, amepewa hifadhi
nchini Niger ambako anaishi katika makao makuu baada ya kutoroka kupitia
jangwa la Sahara.
Saadi ana sifa tata ambapo alikuwa akicheza soka
katika ligi ya Italia ingawa safari yake ilikatizwa baada ya kuhusishwa
na madawa haramu pamoja na maisha yake ya anasa.
Niger imekataa ombi la Libya kumpeleka nchini humo huku waziri wa sheria akisema kuwa huenda akahukumiwa kunyongwa.
Mnamo mwezi Septemba, shirika la Polisi wa kimataifa Interpol lilitoa onyo ambalo litawaruhusu nchi wanachama kamkamata Saadi.
Mwezi Disemba mwaka jana polisi nchini Mexico
walisema wana taarifa za kijasusi kuwa magenge ya wafanyabiashara haramu
ambao wanajaribu kumhamisha Saadi nchini Mexico kwa kutumia stakabadhi
bandia.
Hannibal Gaddafi (Mwanawe Gaddafi)
Hannibal ni mtoto wa tano wa Gaddafi na Safiya
Farkash. Inaamini alikuwa kwenye msafara wa magari ya Gaddafi uliokuwa
unaelekea nchini Algeria mwaka Jana .
Alikuwa anaongoza majeshi kulinda eneo la Gharyan, Kusini mwa Tripoli, kabla ya waasi kudhibiti Tripoli.
Alisifika kwa tabia zake za anasa na aliwahi kukamtwa akiwa amelewa wakati akiendesha gari aina ya Porsche mjini Paris.
Alizua mgogoro wa kidiplomasia na Uswizi baada
ya kuwashambulia wafanyakazi wawili wa hoteli nchini humo na kusababisha
babake kuwafunga jela wafanyakazi kutoka nchini humo, na hata kuiwekea
nchi hiyo vikwazo.
Aisha Gaddafi (Mwanawe Gaddafi wa kike)
Mwanawe pekee wa kike alipewa hifadhi nchini Algeria pamoja na mamake na ndugu yake.
Licha ya kuwekewa ulinzi mkali na serikali ya
Algeria, aliripotiwa hivi karibuni kuwataka watu nchini Libya kupindua
serikali ya sasa. Kwa usaidizi wa wakili wake Muisraeli, aliitaaka
mahakama ya ICC kuchunguza kifo cha babake
Aisha pia aliripotiwa kuunga mkono Algeria
katika mechi moja kati yake na Libya akisema kuwa serikali mpya ya Libya
haimwakilishi kivyovyote.
Hanaa Gaddafi (Mwanawe wa kuasiliwa)
Kanali Gaddafi alikuwa kwa muda mrefu akidai
kuwa Hanaa aliuawa katika shambulizi la Marekani mwaka 1986 wakati akiwa
na mwaka mmoja na nusu. Lakini tangu mapinduzi kufanyika, kumekuwa na
taarifa kuwa Hanaa yuko hai ingawa hajulikani aliko.
Moussa Ibrahim (aliyekuwa msemaji wa Serikali)
Tarehe 20 mwezi Oktoba, mwaka mmoja baada ya
kifo cha Gaddafi, taarifa kutoka kwa ofisi ya waziri mkuu zilisema kuwa
Ibrahim alikamatwa na waasi mjini Tarhouna, maili arobaini kutoka mji
mkuu.Maafisa wengine hata hivyo walishuku habari hizo.
Kumekuwa na taarifa nyingi kuhusu kukamatwa kwake lakini baadaye ikasemekana kuwa uongo.
Alikuwa mwsemaji wa serikali na kujulikana na
vyombo vya habari vya kimataifa, alionekana mwisho mjini Tripoli kabla
ya waasi kuudhibiti mji huo.
Kila siku alitoa taarifa kwa waandishi wa habari
kuwahakikishia kuwa serikali itaendelea kuwa imara na kwamba waasi
hawatafanikiwa kuiangusha.Alitoka kabila moja na Gaddafi na alijigamba
kuishi nchini Uingereza kwa miaka 15 kabla ya kurejea nyumbani.
No comments:
Post a Comment