Pages


Photobucket

Monday, October 29, 2012

TAARIFA MBALIMBALI ZA MATOKEO YA CHAGUZI MBALIMBALI ZA UDIWANI OKTOBA 2012


Matokeo ya Uchaguzi wa Udiwani Kata ya Daraja Mbili

Katika matokeo kamili ya uchaguzi wa Udiwani wa kata ya Daraja Mbili, CHADEMA wameweza kushinda kwa kupata kura 2193 , CCM kura 1324, CUF kura 162, TLP kura 42 na NCCR mageuzi kura 22.

Waliojiandikisha ni wananchi elfu kumi na sita mia mbili tisini na tano, waliopiga kura wapo 3,770, zilizo halali ni kura 3,743 na zilizoharibika ni 27.

Picture
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willbrod Slaa akijumuika kucheza ngoma ya kisukuma iliyokuwa ikitumbuizwa na katika Kijiji cha Lubili, Misungwi, Mwanza. Dkt. Slaa alifika kijijini hapo akiwa katika mizunguko ya mikutano ya kampeni za uchaguzi mdogo wa Kata ya Lubili. Anayeonekana kushoto akishangilia kwa kupiga makofi ni Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere.

BASTOLA NJE NJE UCHAGUZI ARUSHA, RISASI ZARINDIMA HEWANI

UCHAGUZI  mdogo wa udiwani katika kata ya Daraja Mbili Mkoani Arusha umeingia dosari baada ya risasi kurindima hewani mfulululizo asubuhi ya Jumapili, Oktoba 28, 2012 karibu na maeneo ya kupigia kura hali iliyozua taharuki kwa wakazi wa kata hiyo waliokuwa wamejitokeza katika vituo vya kupigia kura.

Risasi hizo zinadaiwa kupigwa na Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilayani Arusha, Godfrey Mwalusamba mara baada ya kuibuka tafrani baina ya wafuasi wa CCM na CHADEMA katika eneo la Shule ya Sekondari ya Felix Mrema.

Katika vurugu hizo, dereva wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Haleluya Natai pamoja na wafuasi wa CHADEMA zaidi ya 15  walikamatwa na jeshi la polisi huku Nasari na aliyekua mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbles Lema wakitokomea kusikojulikana lakini baadaye walionekana katika viunga vya kupigia kura.

Hatahivyo, katika hali isiyo ya kawaida naye mgombea wa CHADEMA katika kata hiyo, Prosper Msofe alionekana akirandaranda katika vituo vya kupigia kura huku akiwa na silaha yake aina ya bastola kiunoni hali ambayo ilizua mshangao kwa wapiga kura wa kata hiyo.

Katika vurugu hizo inadaiwa kuwa Nasari aliyekuwa akiongozana na Lema wakiwa katika gari mojawapo, walivamia ngome ya CCM iliyopo karibu na ofisi za chama hicho kata ya Daraja Mbili hali ambayo ilisababisha wafuasi wa CCM kuwavamia lakini Nasari alijiami na kisha kufyatua risasi tatu hewani.

Katika purukushani hiyo, kada wa CCM , Kabwelwa Mturuka alijeruhiwa mkononi kwa kukatwa na panga na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa CHADEMA wakati wa majibizano karibu na kituo cha kupigia kura.

Katika  vurugu hizo mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arusha, Martin Munisi naye aliporwa simu yake ya mkononi na fedha ambapo  alitoa taarifa kwa jeshi la polisi na kupewa AR/RB/13624/2012 ya shambulio la kudhuru mwili dhidi ya Nasari na Lema.

Wakati huohuo,wafuasi wa CHADEMA waliokuwa meta chache karibu na kituo cha kupigia kura cha Sekondari ya Felix Mrema baada ya zoezi la uchaguzi kwisha, wakati wakisubiri matokeo, walivamia ofisi za CCM zilizokuwa karibu na kituo hicho na kisha kujaribu kung’oa bendera ya chama hicho lakini jitihada hizo zilizimwa na wafuasi wa CCM baada ya kumshusha kabla hajaikaribia bendera hiyo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas alipoulizwa juu ya matukio hayo alisema kwamba ni mapema sana kuzizungumzia lakini alikiri kushikiliwa kwa baadhi ya wafuasi wa CCM na CHADEMA ambao walihusika na vurugu katika uchaguzi huo.

Kwa upande wake,Nasari alipoulizwa juu ya hatua yake ya kurusha risasi hewani alipinga vikali lakini alipotafutwa Mwalusamba alikiri kurusha risasi hizo hewani huku akidai kwamba alifyatua kwa lengo la kujihami.
  Aidha saa nne usiku matokeo yamekemilika na kutangazwa na Modest Lupogo kwa niaba ya kaimu mkurugenzi wa jiji la Arusha Omary Mkombole ambapo alisema kuwa idadi ya watu walioandikishwa kupiga kura ni 16295 lakini waliojitokeza kupiga kura ni 3770 tu.

Akitangaza mshindi (Diwani mpya wa Kata ya Daraja Mbili) Lupogo alisema kuwa Prosper Msofe aliibuka kidedea kwa kura 2,193  kupitia CHADEMA, akifuatiwa na mpinzani wake Philip Mushi Philip kupitia CCM aliyepata kura 1,324, huku CUF ikipata kura 162, TLP wakipata kura 42, na NSSR kuambulia kura 22.

Wakati huo huo, katika kata ya Bangata iliyoko wilayani Arumeru mkoani Arusha, akitangaza matokeo hayo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Halipha Idda alisema kuwa Olais Peter kupitia CCM ameibuka kidedea kwa kura 1,177 na kuwaacha wapinzani wake Erick Samson Mollel kupitia CHADEMA kwa kura 881 huku Samweli Simon Ndosi kupiti TLP akiambulia kura 3.

CCM YAIBWAGA CHADEMA BUGARAMA, KAHAMA

Picture
Kampeni za CCM za Udiwani Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga, Oktoba 27, 2012
Chama cha Mapinduzi kimefanikiwa kuibwaga CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa Udiwani uliofanyika katika Kata ya Bugarama wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Habari zilizopatikana zimesema,  katika uchaguzi huo ulifanyika leo CCM imepata kura 1145
CHADEMA: 772 na TADEA: 156 wagombea wakiwa Nixon Igoko (CCM) Erasmus Francis (CHADEMA) na Clement Michael (TADEA) .

Pia habari zilizopatikana kutoka Kata ya Shinyanga mjini ambako pia uchaguzi mdogo wa Udiwani umefanyika, zimasema CCM imeshinda. Hata hivyo hatukuweza kupata mizania ya ushindi huo kwa kura.

Picture
Kampeni za CCM za Udiwani Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga, Oktoba 27, 2012
Picture
Kampeni za CCM za Udiwani Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga, Oktoba 27, 2012

CHADEMA YAITOA JASHO CCM

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeendelea kukipa wakati mgumu Chama cha Mapinduzi (CCM) katika siasa, ambapo kwenye matokeo ya udiwani katika uchaguzi uliofanyika leo, chama hicho kimefanikiwa kutetea kata zake na kunyakua nyingine za CCM.

Hata hivyo uchaguzi huo ambao ulifanyika kwenye kata 29 katika halmashauri mbalimbali nchini, umemalizika huku vurugu kubwa zikitawala na kusababisha wafuasi wa vyama hivyo kuumizana.

Hadi sasa matokeo ya kata 14 yanaonyesha kuwa CCM ilikuwa imefanikiwa kurejesha kata zake saba, huku CHADEMA ikinyakua kata sita, ambapo mbili zilikuwa za kwao na nne imewanyang’anya CCM na CUF ikiwa na kata moja.

Matokeo ya udiwani katika baadhi ya kata yalikuwa yakiendelea kutolewa huku CHADEMA ikiendelea kuikaba CCM kwa kuzitwaa baadhi ya zilizokuwa kata zake.

Jijini Arusha katika Kata ya Daraja Mbili, CCM ilipoteza kata hiyo kwa CHADEMA iliyozoa kura 2192 dhidi ya 1315 za chama tawala.

CHADEMA wameweza kuzirejesha kata zao mbili za Nangerea jimboni Rombo, ambapo mgombea wao Frank Sarakana alijizolea kura 2370 dhidi ya 1134 za Dysmas Silayo wa CCM pamoja na ile ya Mtibwa, mkoani Morogoro.

Wilayani Sikonge katika kata ya Ipole, CCM walipoteza kata hiyo kwa CHADEMA iliyopata kura 577 dhidi ya 372 za washindani wao, na vilevile kuitwaa kata nyingine ya Lengali wilayani Ludewa iliyokuwa ya CCM.

CHADEMA pia ilikuwa ikiongoza katika kata ya Mpwapwa, mkoani Dodoma, hadi tunakwenda mitamboni usiku.

Nayo CCM ilifurukuta kwa kuzirejesha kata zake za Msalato ya mkoani Dodoma, Bang’ata ya Arumeru Magharibi kwa kuwa 1177 dhidi ya 881 za CHADEMA, Mletele ya Songea CCM ilishinda kwa kura 950 na CHADEMA ilipata 295.

Pia CCM iliweza kutetea kata zake za Mwawaza mjini Shinyanga, Lwenzela mkoani Geita, Bungala wialayni Kahama na Bagamoyo mkoani Pwani kwa kuibwaga CHADEMA wakati Chama cha Wananchi (CUF) kilishinda kata ya Newala.
Picture
Mfuasi wa CHADEMA akiwa na majeraha kichwani baada ya kushambuliwa na watu wanaodhaniwa kuwa vijana wa CCM katika kituo cha kupigia kura Jijini Arusha kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya daraja Mbili Manispaa ya Arusha.

CCM KATA YA MLANGALI LUDEWA NO, CHADEMA YES

Katika  kuonyesha  kuwa  chama cha mapinduzi (CCM) hakikubaliki katika kata ya Mlangali  wilaya ya Ludewa mkoani Njombe ni baada ya  wapiga kura  wa kata hiyo kumgalagaza vibaya mgombea  wa Chama  cha mapinduzi (CCM) Andrew Mhagama  na kumchagua na kumchagua mgombea wa CHADEMA Faraja Mlelwa wa CHADEMA.
katika  uchaguzi huo  mgopmbea  wa CHADEMA Bw. Faraja ameshinda kwa tofauti ya kura 163 dhidi ya mgombea  wa CCM mzee Mhagama na hoja kubwa ya kufanya wapiga kura  kutomchagua Mhagama ni kuwa ni mzee ambaye itakuwa  vigumu kufanyakazi na mbunge wa  jimbo  hilo Deo Filikunjombe (CCM) ambae ni kijana .

CCM YASHINDA UDIWANI SONGEA

Chama cha Mapinduzi kimefanikiwa kutetea kiti chake cha Udiwani katika kata ya MLETELE iliyopo katika manispaa ya SONGEA Mkoani RUVUMA baada Mgombea wa kiti hicho MAURUS LUNGU kwa tiketi ya CCM kushinda katika uchaguzi mdogo uliofanyika Jumapili.

Akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo mdogo, msimamizi wa Uchaguzi huo ZAKARIA NACHOA amesema MAULUS LUNGU amepata kura 955 akiwapiga mweleka Mgombea wa Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA LEOCARDO MAPUNDA aliyepata kura 297, Mgombea SALUM CHALE wa Chama Cha Wananchi CUF aliyepata Kura 27.

Uchaguzi huo umefanyika kwa lengo la kuziba nafasi ya aliyekua diwani wa kata hiyo FLAVIAN LEGELE ambaye alifariki Dunia

Hata hivyo Uchaguzi Mdogo wa kata ya MLETELE uliingia doa siku moja kabla ya siku ya Uchaguzi baada ya wafuasi wa Vyama viwili vilivyokua na upinzani mkubwa, CHADEMA na CCM kushambuliana kwa mapanga ambapo watu sita wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa Mjini SONGEA kwa Matibabu

Miongoni mwa waliojeruhiwa na kulazwa Hospitali ni NYENJE ALLY MPONJI (32), MASHAKA MBAWALA (45) na THABIT SULEIMAN (29) waliojeruhiwa kichwani mikononi na miguuni.

Wengine ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mtaa wa Changarawe aliyeshambuliwa kwa kipigo na majeruhi wengine walitibiwa na kuondoka.

Chanzo cha vurugu hizo ni wafuasi wa vyama hivyo kukutana katika eneo la Kanisani na kuanza kushutumiana, ndipo mashambulizi yakaanza katika gari mojawapo lililokuwepo eneo la tukio. Mapigano yalipoanza na haikujulikana silaha aina ya mapanga, fimbo, mawe na magongo yalikotoka na kuanza kutumika katika mapigano hayo.

---
Chanzo cha taarifa: Ni kwa hisani ya blogu mbalimbali

1 comment: