Pages


Photobucket

Saturday, October 13, 2012

BREAKING NEWS: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA AUWAWA NA MAJAMBAZI USIKU WA KUAMKIA LEO



Katika hali isiyokuwa ya kawaida kamanda wa polisi mkoa wa mwanza  SACP LIBERTUS  BARLOW (Pichani)  ameuwawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi katika eneo la kitangili jijini mwanza usiku wa kuamkia leo.
 
Taarifa kutoka Mwanza ambazo zimethibitishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, zinasema kuwa  kamanda  huyo wa polisi ameuwawa na  watu  wanaosadikika kuwa ni majambazi majira ya saa 7.30  na saa 8 usiku   katika maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza.

Mwema amesema  kuwa kamanda  Barlow alikuwa akitokea katika  kikao cha harusi akiwa njiani kumrudisha dadake nyumbani kwake ghafla  alikutwa na tukio  hilo la  kupigwa  risasi.

Hata  hivyo Said Mwema alisema  kuwa  kutokana na tukio  hilo jeshi la  polisi  linataraji kuanza uchunguzi  wake kuanzia leo na timu ya askari  kutoka  makao makuu ya polisi  wataondoka mapema leo kwenda  jijini Mwanza  kuungana na askari wa mkoa  huo kwa ajili ya uchunguzi  zaidi na msako wa majambazi hayo .

Mwema amewataka  wananchi  wa Mwanza  kutoa ushirikiano wao kwa  jeshi la polisi ili kufanikisha  zoezi hilo na  kuwataka kutokuwa na hofu  yoyote kutokana na tukio  hilo.

No comments:

Post a Comment