Wateja wakubwa wa mapipa laki mia moja na themanini
ya mafuta yanayoibwa kutoka nchini Nigeria wako katika nchi za Kusini
Mashariki mwa Ulaya pamoja na Singapore, kulingana na wanaharakati.
Mwanasiasa kutoka jimbo lenye utajiri wa mafuta
la Niger Delta, Patrick Dele Cole, amesema kuwa asilimia tisini ya
mafuta yanayoibwa yanasafirishwa kwenda nje ya nchi kinyume na sheria.
Amezindua kampeini yenye kauli mbiu ''Komesha wizi'' ili kumaliza visa vya wizi wa mafuta.
Nigeria ni mojawapo ya nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi ingawa idadi kubwa ya wananchi wake wanaishi kwa umaskini
Kampeini hiyo inalenga kuzichunguza meli hizo kwa satelite na kubaini pesa zinazotokana na uuzaji huo zinakokwenda.
''Unapoanza kuuliza maswali, na kuanza kuangazia
swala hili, utakuwa umesuluhisha zaidi ya asilimia hamsini ya matatizo
kuhusiana na wizi wa mafuta.'' alisema bwana Dele Cole, mwanadiplomasia
mkongwe na mshauri wa zamani wa rais.
''Nadhani ni mumimu kutoa onyo kwa wale matajiri kwamba siku yao ya kuwajibika itafika''
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa sekta nzima ya mafuta nchini humo inakumbwa na ufisadi,
Wanasiasa wengi wanahusika na wizi huo anasema
Will, huku sehemu ya mapato ya mafuta hayo yakitumiwa kununua kura na
kufadhili kampeini zao.
Jeshi la Nigeria linapaswa kusitisha visa vya wizi wa mafuta lakini wao huchukua hongo ili kutofuatialia visa hivyo
****chanzo na habari ni BBC****
****chanzo na habari ni BBC****
No comments:
Post a Comment