Pages


Photobucket

Wednesday, October 17, 2012

JINSI WAJUMBE WA CCM WALIVYOPATA AJALI NA MTU MMOJA KUFARIKI DUNIA

                                            Askari wa  usalama barabarabani wakipima ajali hiyo   
                Basi lenye namba za usajili T 853 BRB lililokuwa na wajumbe hao likiwa katikati ya barabara 
Ni ajali ya  basi lililobeba wajumbe wa mkutano mkuu CCM wilaya ya Kwimba, ambapo basi lao lilipata ajali na kuanguka eneo la Buhongwa wilaya ya Nyamagana, mkoani Mwanza  majira ya saa 3:30 - 4:00 asubuhi(jana Tarehe 16/10/2012) ambapo inatajwa kuwa dereva wa chombo hicho cha usafiri alifariki dunia papo hapo na wajumbe wengine saba kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali ya rufaa Bugando.


Chanzo cha ajali hiyo kinatajwa kuwa basi hilo lililokuwa katika mwendo kasi lilikuwa katika harakati yakulikwepa roli aina ya fuso ambalo lilikuwa likigeuza kujiweka sawa kuingia barabarani ndipo basi hilo lilipopoteza uelekeo na kulibamiza fuso na kupinduka.

Wajumbe hao kutoka wilaya ya Kwimba, walikuwa wakiingia jijini Mwanza kwenye uchaguzi wa viongozi na wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mwanza iliofanyika jana  uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.  
   ****Mwandishi  Maalum-Mwanza***

No comments:

Post a Comment