Saif al-Islam
Mahakama ya kimataifa ya jinai ICC hii leo inafanya 
kikao cha kwanza mbele ya umma dhidi ya mwanawe aliyekuwa Rais wa Libya 
Muamar gaddafi,Saif Al Islam.
Saif anatuhumiwa kwa kuhusika na uhalifu wa kivita dhidi ya waasi waliopindua serikali ya babake mwaka jana.
Hata hivyo tofauti zimeibuka kuhusu ikiwa kesi yake iendeshwe Libya au katika mahakama ya ICC mjini The Hague.
Mawakili wake wanatarajia kupinga pendekezo 
lolote la kesi yake kusikilizwa Libya wakisema kuwa hatapata hukumu ya 
haki nchini humo.
      Saif al-Islam   
(Picha ilichukuliwa March 10, 2011)
Hata hivyo maafisa wakuu nchini humo wanataka kesi yake iendeshwe nchini humo.
Katika siku ya kwanza ya kikao hicho, wakili wa 
Libya Ahmed al-Jehani ameitaka jamii ya kimataifa kuwa na uvumilivu 
akiwataka majaji wa mahakama hiyo kuelewa kuwa maafisa wa Libya 
wanahitaji muda zaidi kuweza kuandaa kesi ya haki dhidi ya Saif Gaddafi.
Bwana Jehani aliwaambia majaji kuwa hawajaondoa uwezekano wa mahakama ya ICC kuhusishwa katika kesi hiyo.
Hii ni mara ya kwanza mawakili wa mahakama ya ICC wameweza kukutana ana kwa ana na mawakili wa Libya mahakamani.
Hata hivyo maafisa wa Libaya wamekuwa wakisema 
kuwa hawako tayari kumkabidhi Saif kwa mahakama ya ICC na kwa hivyo 
lazima wawashawishi majaji kuwa Gaddafi atatendewa haki nyumbani.
Lazima waonyeshe kuwa wanafanya uchunguzi wao 
binafsi na wana nia ya kumfungulia Saif mashtaka sawa na yale ambayo 
yako kwenye kibali cha kumkamata ambayo ni ya uhalifu wa kivita.



No comments:
Post a Comment