Pages


Photobucket

Tuesday, October 30, 2012

JOSHUA NASSARI AKANUSHA KUFYATUA RISASI KWENYE UCHAGUZI WA MADIWANI DARAJA II ARUSHA JUZI

Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Mh Joshua Nassari alikanusha taarifa zilizoandikwa na magazeti ya Uhuru na Habari jana kuwajuzi alifyatua risasi na kuzua tafrani katika uchaguzi wa kumtafuta Diwani wa Kata ya Daraja Mbili ya Jijini Arusha, uchaguzi uliofanyika juzi ambapo mgombea wa Chadema aliibuka mshindi.
Nassari ameyasema hayo jana  jioni wakati akihutubia katika Mkutano wa hadhara kuzindua kampeni nyingine za chama chake kwa ajili ya chaguzi za Serikali za Mitaa kwa ajili ya Halmashauri ndogo ya Mji wa Usa River unaotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo ya Novemba 4, 2012.
Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na watu wengi, ulifanyika katika viwanja vya Ngaresero Usa-River ambapo mbali na Nassari, Katibu wa CHADEMA Kinondoni Ng Henry Kileo nae alikuwepo na alipewa nafasi ya kuzungumza.
Nassari alidai kuwa katika uchaguzi wa juzi yeye alikuwa Wakala Mkuu wa CHADEMA Kata ya Bangata na hivyo kumhusiha na ya Daraja Mbili haelewi inakujaje. Amedai kuwa mtu aliyefyatua risasi ni Mwenyekiti wa UVCCM, Godwin Mwalusamba na kwamba Polisi walimuweka ndani na kuandika maelezo yake, lakini anashangaa kuambiwa ni yeye wakati siyo!
Akifafanua zaidi aliviomba vyombo vya usalama avinavyohusika na masuala ya vibali vya kumiliki silaha za moto, kufanya uchunguzi wao na waeleze hiyo bunduki walimpa lini na ni risasi zimetumika, na kwamba kama ni kumkamata yeye yupo huru muda wowote wanaweza kumkamata.
DSCN5926Mh Nassari akihutubia mkutanoni hapo jana
DSCN5946Sehemu ya umati ulijitokeza katika ufunguzi huo uliofanyika katika uwanja wa Ngaresero, Usa-River
DSCN5906Katibu wa CHADEMA Kinondoni, Dar es Salaam, Henry Kileo akizungumza na wananchi wa Usa River leo jioni.Nassari alisema kampeni hizo zitahitimishwa Novemba 3, 2012 katika viwanja hivyo na kuna uwezekanao Mh Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Chama hicho taifa akahudhuria.

Awanadi wagombea wa Chadema
DSCN5952Mh Nassari aliweza kuwatambulisha rasmi wagombea wa Chama chake (waliosimama) watakaoshiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 9 katika Halmashaur ya Mji Mdogo wa Usa River, uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Jumapili ya Novemba 4, 2012. Katika wagombea hao, mwanamke aliyejitokeza ni mmoja tu, Verian Mushi ambae anagombea mtaa wa Magadini.

Wagombea wa Chadema na Mitaa wanayogombania ni hawa wafuatao
1. Verian Mushi – Magadini,

2. Henry Benjamin Mpinga – Manayata
3. Ernest Makalla Shilla – Magadirisho
4. Exaud Jackson Mbise – Nganana
5. Richard Mohamed Ngungu – Kisambare
6. Malisa – Mji Mwema
7. Santrumini Filipo – Mlima Sioni (Lake tatu)
8. Frank Anael Msuya – Usa Madukani
9. William – Ngarasero
DSCN5908Baadhi ya viongozi wa Chadema Usa River na wagombea wao

Nassari azungumzia mafanikio ndani ya miezi 5 ya ubunge wake
Katika hotuba yake, Mh Nassari aliweza pia kuzungumzia baadhi ya mambo ambayo amekwishayafanya kwa wananchi wake wa Arumeru tangu wamchague kuwa mbunge wao, takribani miezi mitano iliyopita.

Akiorodhesha mambo hayao harakaharaka, Nassari alisema kwamba amekwishakamilisha mradi wa majai ya kisima wenye thamani ya sh mil 60 kwa maeneo ya Ngobobo na Ngarenanyuki.
Akaeleza kuwa ameanzisha ligi ya mpira wa miguu kwa Kata zote za Jimbo lake ambapo amedai kuwa vifaa vimemgharimu zaidi ya sh milioni 5. Ligi hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 10 Novemba, 2012.
Alidai kuwa ameshiriki kwenye harambee nyingi za maji na kwamba ya karibuni amechagia kiasi cha sh milion 1.5, pia amechangia sh milioni 1 kwaya ya Jimboni kwake iliyomwaomba kuwasaidia.
Mambo mengine ni pamoja kusambaza vitabu vyenye thamani ya sh milion 38 kwa shule 15 za Kata, sehemu kubwa ikiwa ni msaada wa rafiki zake wa Marekani. Pia nmatengenezo ya choo kwa shule ya msingi Liganga, kuchangia vikundi vya kina mama.


CHANZO;  NOISE OF SILENCE BLOG

No comments:

Post a Comment