Pages


Photobucket

Monday, October 15, 2012

MH: DKT HAMISI KIGWANGALLA: NITAGOMBEA URAIS MWAKA 2025



Akiwahutubia wananchi wa Nzega siku chache zilizopita  Mbunge wa jimbo la Nzega kupitia tiketi ya CCM Dkt Hamisi Kigwangalla ametangaza kuwa na ndoto za kuwania Urais 2025! Alisema:
'Kwa hakika dunia inakuwa mahala. Pabaya pa kuishi si kwa sababu ya watu wabaya bali kwa sababu ya ukimya wa watu wazuri..watu safi na wazuri kama mimi, japokuwa tuko wachache, ni lazima tujipange na tusimame imara kuutafuta uongozi wa nchi yetu la sivyo kundi kubwa la watu wabaya litatutawala na tutabaki tukisaga meno - wanaodhani watanitoa ubunge kirahisi wanaota ndoto za fisi, wanamsubiri nyuma  mtembea kwa miguu wakidhani atadondosha mkono, sina mpango wa kuachia ubunge hata kidogo, wajiandae kupambana na mimi ndani ya chama na hata wale wa upinzani na nina hakika nitawashinda tu, maana safari hii haikomi mpaka 2025 nitakapogombea Urais'


Alitoa kauli hiyo huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wapiga kura wake. "Sikuwahi kujua kama huyu Mbunge anapendwa na watu wake namna hii!! Wamemshangilia mpaka nikaogopa. Anaongea kwa kujiamini sana kiasi cha kumuaminisha kila anayemsikiliza" Mmoja wa watu waliohudhuria alisikika akisema.

No comments:

Post a Comment