Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, amewataka
wafanyakazi wa migodini kurejea kazini baada ya migomo iliyokumbwa na
ghasia.
Baada ya mkutano wa masaa tano na viongozi wa
vyama vya wafanyakazi, bwana Zuma alitoa wito wa kutaka uzalishaji wa
madini migodini kurejealea hali yake ya kawaida.
Zuma pia amewataka vwafanyabiashara wakuu nchini humo kutojilipa mishahara angalau kwa mwaka mmoja.
Uzalishaji wa madini nchini Afrika Kusini,
umekumbwa na migomo mingi ambayo ilisababisha mauaji ya wachimba migodi
zaidi ya arobaini.
Kampuni ya madini ya Anglo American Platinum wiki jana iliwafuta kazi wachimba migodi 12,000 waliokuwa wanagoma.
Kampuni ya Amplat ndiyo mojawapo ya makampuni makubwa ya kuchimba madini duniani.
Wachimba migodi 15,000 katika mgodi wa Gold
Fields, ambayo ni ya nne kwa ukubwa zaidi kuzalisha dhahabu duniani,
huenda wakafutwa kazi ikiwa hawatarejea kazini saa nane mchana wa leo.
"Tukubaliane kuanzia sasa kuwa lazima ghasia
zikome. Ghasia hazina nafasi katika mfumo wetu na pia zina athari kubwa
kwa kazi zetu'' alisema bwana Zuma
Pia aliwataka wakurugenzi wakuu kusimamisha
mishahara yao na marupurupu yao ya mwaka ujao ili wachangie katika
kujenga nchi yenye uchumi thabiti.
Kauli ya Zuma ndiyo ya kwanza nzito tangu kuanza kwa vurugu migodini.
*****CHANZO CHA HABARI HIZI NI - BBC*****
No comments:
Post a Comment