Pages


Photobucket

Wednesday, October 10, 2012

SIZ KITAA YA CLOUDS TV YAIBUA MENGI : MAGUFULI NA SLAA WAONEKANA KIPENZI CHA VIJANA.



               CASTO DICKSON  -  MUENDESHA KIPINDI  CHA SIZ KITAA (CLOUDS TV)
Waziri wa  Ujenzi Mh. John Magufuli  na  Katibu Mkuu wa CHADEMA  Dk.Willibrod  Slaa  wameonekana kuwa kipenzi kikubwa cha vijana,Hatua hii imefikiwa kupitia kipindi cha Clouds TV kinachoendeshwa na Bw. Casto  Dickson  leo  mnamo saa sita mchana wakati akiwa  jijini Dar es salaam   wilaya ya kinondoni, Eneo la Manyanya , Mahali ambapo  katika kuendesha kipindi chake alikukutana na vijana mbalimbali  ambapo kwa mujibu wa mada ya siku ya leo aliwataka vijana hao kuwataja baadhi ya watu maarufu nchini na Duniani kote ambao wanakubalika kupitia  shughuli zao.
                                       WAZIRI WA UJENZI  DK. MAGUFULI

Kwa upande wa vijana hao ambao wengi wao walikuwa ni Madreva wa Tax na Bajaji  wamemtaja Waziri Magufuli kama  Ki ongozi anayejituma katika harakati za kuwatumikia watanzania wote kupitia  wizara yake.Katika hatua nyingine Dk.Slaa ameonekana  kuungwa mkono na kundi hilo la Vijana ambapo wengi wao wamemtaja kama mtu anayepigania watanzania  kupitia wadhifa wake alio nao.
Wengine waliotajwa katika anga za kisiasa ni Mh Zitto Kabwe na January Makamba ambao pia wameonekana kuwa kipenzi kikubwa  kwa vijana kupitia utendaji wao.

 DK. SLAA

Wakiwataja watu Maarufu,wengine  katika anga ya Michezo  Mchezaji  ni Lionel Mess (Barcelona),Didier Drogba (Shanghai Shenhua Kelvin Yondani (Yanga) na  John Rooney (Man United)  kwa upande wa Wanamziki vijana hao  wamemtaja  Msanii Juma Nature  na  Msanii   Rick Ross kutoka Marekani. Hivyo ndivyo vijana waliopata fursa ya Kuzungumza na Bw. Casto wa CLOUDS TV walivyoweza kutoa mitazamo yao.



*******CHANZO CHA HABARI NI CLOUDS  TV*****


No comments:

Post a Comment