Mzee mmoja katika kijiji cha
Bundibugyo(Nchini Uganda), Iddi Mulangira(Pichani mkono wa kulia) amezua mshangao mkubwa kwa wakazi wa kijiji
hicho baada ya kuonekana akisoma katika shule ya Msingi Boma .
Mzee huyo mwenye umri wa
Miaka 63 alisema kuwa ameamua kuanza tena mafunzo tena
katika shule hiyo ili aweze kujifunza somo la kingereza kwa lengo
la kumsaidia katika kusoma nyaraka mbalimbali.
"Nimeamua kurudi tena
darasani ili niweze kujifunza somo la kingereza kwa kuwa
najua litanisaidia katika kutafsiri nyaraka ambazo napewa
ofisini" alisema Mulangira
Aliongeza kuwa anaamini
kurudi darasani kutamsaidia katika kusimamia familia
yake kwa kuwa kusoma kutamwezesha kuwa na usimamizi
mzuri wa fedha na biashara zake .
Mulangira ambaye anafanya kazi ya
kubeba mizigo katika makao makuu ya wilaya hiyo alisema
kuwa amefanya kazi hiyo kwa muda wa miaka 30, jambo ambalo
limemsababisha kuchoshwa na kazi hiyo ya ubebaji wa mizigo.
"Sipendi kuendelea na kazi
hii ya ubebaji mizigo ndiyo maana nimeamua kwenda shule kwa sababu
nina imani nikipata elimu naweza kuwa msimamizi mkuu na mshahara wangu
ukaongezeka "alisema .
Alisema kuwa rafiki yake
ambaye alikuwa akisoma kitabu cha haki za binadamu alimvutia
na kusababisha kujiunga na elimu ya msingi kwa lengo la kupata
elimu zaidi .
"Rafiki yangu alikuwa akisoma
kitabu cha haki za binadamu baada ya hapo aliniomba niandike jina
langu,baada ya kushindwa ndipo alinishauri niende nikasome kwa kuwa ni
haki yangu kupata elimu",alisema Murangira.
Aliongeza kuwalicha ya
kufanikiwa kusoma katika shule hiyo bado anakumbana na changamoto nyingi
ikiwamo kukosa chakula cha mchana hali ambayo inamsababisha
kukaa na njaa kwa muda mrefu.
Baada ya kukaa shule kwa miezi minne
mzee huyo kwa sasa anaweza kuandika jina lake na kiwango chake cha
kusoma na kuandika kimekua.
"Kabla ya kwenda shule nilikuwa najua
kusalimia na baadhi ya maneno kidogo kama
kikombe,kalamu,lakini sasa nafahamu mambo mengi nawasifu sana walimu wa shule
hii ", alisema.
No comments:
Post a Comment