Mkazi wa kashmir,nchini India ,Mohammad Latif Khatana (Pichani) Amejitokeza hadharani kwa mara ya kwanza na kuzungumza juu ya ugonjwa wa ajabu unaomsumbua , ambao umeziba kabisa sura yake. kutokana na ugonjwa huo Khatana mwenye umri wa miaka 32 sasa hana uwezo wa kuona ,wala kufanya kazi pamoja na kuwa katika hali hiyo Khatana amepata mke ambaye ana mimba ya miezi saba ingawa bwana huyo anayo hofu juu ya mtoto wake kuweza kupata ugonjwa huo.
"Nasubiri kuwa baba na kuwa na furaha kama wanaume wengine ,lakini nakuwa mwoga siku baada ya siku na ninamuomba Mungu mtoto wangu asifanane na mimi.alisema Khatana.
Latif ,anaishi katika Milima ya Tuli Bana katikati ya jammu na kashmir na mke wake salima mwenye umri wa miaka 25 ,husafiri kwa muda wa miezi minne kila mwaka kwa ajili ya kwenda mjini kuombaomba fedha.
Katika historia yake alizaliwa na donge dogo juu ya paji la uso lakini liliendelea kukua mpaka kuunda nyamanyama ambazo zimeziba sura yake.Anasema siku zote mama yake amekuwa akilia.Tangu utoto wake alikuwa akitengwa na jamii iliyomzunguka.
Akiwa na umri wa miaka minne alipoteza jicho lake moja (la kushoto), na hivyo wenzake walimzomea na kumuita "jicho moja" pamoja na hayo mke wake naye ni mlemavu kwani anao mguu mmoja.Yeye na mke wake huyo wamekuwa wakiishi kwa furaha siku zote.
BW.KHATANA ALIVYO SASA
No comments:
Post a Comment