Rais wa Lebanon Michel Suleiman na waziri mkuu Najib Mikati
Marekani imesema kuwa iko tayari kuchunguza shambulizi la bomu lililomuua mkuu wa ujasusi nchini Lebanon.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, waziri wa
mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton pamoja na waziri mkuu wa
Lebanon Najib Mikati wamekubaliana kuhusu uchunguzi wa pamoja
Wissam al-Hassan na watu wengine saba waliuawa katika shambulio la bomu Ijumaa iliyopita.
Makabiliano yalizuka baada ya mazishi ya afisaa huyo siku ya Jumapili, huku waaandamanaji wakimtaka bwana Mikati kujiuzulu.
Mjini Beirut, Polisi waliwafyatulia risasi na
gesi ya kutoa machozi waandamanaji hao walipokuwa wakijaribu kuvamia
ofisi za serikali mjini humo.
Kuna ripoti kuwa huenda ghasia zaidi zikatokea Kusini na Magharibi mwa Beirut.
Viongozi wa upinzani wamelaumu nchi jirani ya Syria kwa mashambulizi hayo.
Maandamano tayari yamefanyika dhidi ya Syria,
nchini Leabanon na nchi washirika wake huku kukiwa na hofu ya kusambaa
kwa vurugu kupitia eneo la mpakani kati ya nchi hizo mbili.
Idadi kubwa ya maafisa katika serikali ya Lebanon wanaunga mkono serikali ya Syria.
Aidha serikali ya Syria imelaani shambulizi hilo
ambalo pia liliwaua walinzi wa bwana Hassan pamoja na mwanamke mmoja
aliyekuwa karibu na eneo la shambulizi.
Mnamo siku ya Jumapili, Bi Clinton alisisitiza
kujitolea kwa Marekani kuhakikisha uthabiti wa Lebanon, uhuru wake na
muhimu kabisa usalama
Clinton ,aligusia umuhimu wa viongozi wa kisiasa
kushirikiana wakati huu ili kuhakikisha hali ya utulivu inaimarishwa na
kwamba wale waliohusika watawajibishwa kwa kuchukuliwa hatua za
kisheria. .
SOURCE: BBC
No comments:
Post a Comment