Pages


Photobucket

Sunday, October 21, 2012

AMISOM itauhama uwanja wa Mogadishu

Mogadishu stadiumKikosi cha amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia, AMISOM, kimekubali ombi la Shirika la Kandanda la Somalia kuhama kutoka uwanja wa mpira wa Mogadishu, ili uwanja huo upate kufanyiwa ukarabati kuweza kutumiwa tena kama pahala pa michezo.
Msemaji wa AMISOM, Kanali Ali Adan Hamud, alisema AMISOM imekaribisha ombi hilo na kwamba AMISOM imeamua kuondoka kwenye uwanja huo ufikapo mwezi wa Disemba mwaka huu.
Uwanja huo umekuwa kambi ya askari wa AMISOM tangu Agosti mwaka jana.
Kabla ya hapo ukitumiwa na wapiganaji wa Al-Shabab na mapambano makali yamewahi kutokea kwenye eneo la uwanja huo.
 
****SOURCE BBC****

No comments:

Post a Comment