Rais wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz, jana 14/10/2012 alipelekwa Ufaransa kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa alipopigwa risasi.
Kabla ya kuondoka kuelekea Paris, Rais Abdel Aziz alisema kwenye
hotuba iliyotangazwa kwenye televisheni kutoka hospitali, kwamba
ameshafanyiwa upasuaji ambao ulifanikiwa.
Wakuu walisema rais alijeruhiwa wakati wanajeshi wa serikali waliokuwa kwenye doria, walipofyatulia risasi msafara wa rais.
Inaarifiwa kuwa maafisa wawili wa jeshi wamekamatwa.
Jenerali Abdel Aziz, ambaye anaonekana na
mataifa ya magharibi kuwa anasimama dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu
katika eneo hilo, alichaguliwa mwaka wa 2009, mwaka mmoja baada ya
kupindua serikali.
No comments:
Post a Comment