Pages


Photobucket

Monday, October 22, 2012

HIVI NDIVYO AJALI ILIYO HUSISHA BASI LA ABIRIA (COSTA) ILIVYO TOKEA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM (KAWAWA ROAD)

Ni katika eneo la  kinondoni B  barabara ya  Kawawa  jana  tarehe 21/10/2012 mnamo mida ya saa tisa Alasiri , Wakati Dereva  wa  gari ya kampuni ya  Soda Pepsi yenye namba T 407 AAY alipo mchomekea kwa mbele dereva wa  gari la Abiria   aina ya Costa  lenye nambari T 462 BFA hatua iliyopelekea  Costa kuligonga kwa nyuma gari la kampuni ya  Pepsi na kuzua tafrani kubwa.Katika tukio hilo  Dereva wa gari la kampuni ya Pepsi alikimbia mara tu baada ya kusababisha ajali na kubaini kwamba yeye ndiye aliyekuwa na makosa.
Katika ajali hiyo dereva wa gari la abiria (COSTA) ambaye jina lake halikufahamika mapema   aliumia sana  pamoja na baadhi ya abiria  waliokuwa wamekaa viti vya mbele, hatua iliyopelekea watu hao kuondolewa katika gari hilo licha ya kukandamizwa na  gari hilo kisha kukimbizwa hospitalini kwa matibabu zaidi.
         Baadhi ya mashuhuda wakitazama jinsi ajali ilivyotokea
       Juhudi za kumtoa dereva wa Costa zikiendelea, ambapo taratibu zilifanyika ili kusogeza mbele gali la Kampuni ya soda pepsi.
Wasamalia wema wakiendelea na juhudi za kunusuru maisha ya Dereva pamoja na abiria walio kuwa wamekaa viti vya mbele
 Wasamalia wema wakiwa wamembeba Dereva wa gari aina ya Costa baada ya kutolewa akiwa mzima licha ya kuwa na majeraha mengi
Dereva huyo akiwa amelazwa katika gari jingine tayari kupelekwa hospitali  yeye pamoja na abiria wengine walio umia katika ajali hiyo.
 Eneo la mbele  la gari aina ya Costa  kama linavyoonekana,huku staring ikiwa imetapakaa damu.
Eneo la nyuma la gari ya  kampuni ya soda ya pepsi kama inavyoonekana baada ya ajali hiyo kutokea.
Baadhi ya Mashuhuda wakiwa  wamekusanyika eneo la tukio.

   


No comments:

Post a Comment