Pages


Photobucket

Saturday, October 27, 2012

KATIKA HILI MH. WAZIRI ALITELEZA KIDOGO (NAYE NI BINADAMU KAMA WALIVYO WENGINE)


NAIBU Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Augustino Mulugo amefunguka kuwaomba radhi Watanzania kwa kujichanganya kwake katika hotuba aliyoisoma kwenye mkutano wa kimataifa nchini Afrika Kusini hivi karibuni.

Katika mkutano huo uliojaa pia Wazungu, waziri huyo alianza kwa kuelezea asili ya nchi yake ambapo alisema Tanzania ni muungano wa Tanganyika, Visiwa vya Bahari ya Hindi, Pemba na Zimbabwe.

Kufuatia kauli yake hiyo, kuanzia Jumatano iliyopita, vyombo vya habari vya ‘elektroniki’ na mitandao mbalimbali ya kijamii Bongo, vimekuwa vikimnanga waziri huyo na kuonekana kauli yake ni aibu kwake na kwa taifa.

Wengi walisema mheshimiwa huyo alikosa umakini, wengine wakadai ni ugeni wa kusimama kwenye majukwaa ya kimataifa na wengine kudai kuwa hajui historia ya nchi yake.

“Waziri mzima hajui Tanzania ni muungano wa nchi zipi jamani? Du! Hii kali. Sasa Zimbabwe imeingiaje kwenye muungano?” msomaji mmoja wa kwenye mtandao alituma maoni hayo.
Juzi Alhamisi, kupitia Kipindi cha Power Breakfast cha Radio Clouds FM, waziri huyo alizungumzia kilichotokea na akawaomba radhi Watanzania kwa kuboronga kwake.

Alisema kabla ya yeye kupanda jukwaani kuhutubia kulikuwa na mwakilishi kutoka Zimbabwe ambaye alizungumza, hivyo yeye alipoanza, kichwani bado alikuwa ana maneno ya aliyemtangulia.
Waziri Mulugo alisema haikuwa makusudi yake kukosea jina la Zanzibar na kutamka Zimbabwe bali kwa vile aliyetangulia alikuwa wa Zimbabwe hivyo neno Zimbabwe lilikuwa karibu sana kwake na kujikuta akitamka Zimbabwe.

“Ilitakiwa baada ya kufika pale umshukuru mwenzako aliyepita, sasa mawazo ndiyo yaliyokuwa yamedhania hivyo kwa sababu nchi zote zimeanzia na Z, lakini nakiri kabisa kwamba sikuwa na makusudi nitamke Zimbabwe,” alijitetea Mulugo.

Kuhusu kukosea kutaja mwaka kwa Kiingereza badala ya nineteen sixty four (1964) na kusema one nineteen sixty four (1,1964), waziri huyo alisema:

“Mimi pale nia yangu ilikuwa ni kusoma digit (tarakimu) mojamojaĘ nikashtukia nakwenda kusoma mbili, haijakaa kama nimekosea Kiingereza kama watu wanavyoipanua kwa mfumo huo lakini kama watu wamenielewa hivyo niombe tu msamaha.”
 KWA HISANI YA GPL BLOG

No comments:

Post a Comment