Pages


Photobucket

Tuesday, October 23, 2012

MWANAJESHI MMOJA AFARIKI DUNIA NA MWINGINE KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA NDEGE YA KIVITA DAR

MWANAJESHI mmoja amekufa na mwingine kujeruhiwa baada ndege ya mafunzo waliyokuwa wakiendesha kushindwa kupaa kwa kujipiga bawa kwenye hanga Uwanja wa Ndege wa Jeshi, Airwing, Ukonga, Dar es Salaam leo.

Akielezea juu ya ajali hiyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kanali Kapambala Mgawe, alitaja jina la aliyepoteza maisha kuwa ni Kapteni Mangushi na aliyejeruhiwa kuwa ni Kampeni Kilikila.

Anasema kuwa wanajeshi hao wanafunzi walikuwa kwenye mafunzo ya kawaida, ambapo waliipanda ndege hiyo ya kivita huku wakiwa na miavuli, na baada ya kuruhusiwa walifyatua kitufe cha kupaa ndege, lakini bahati mbaya ilishindwa kwenda angani na paa lake kugonga hanga la kutengenezea ndege. Ndege hiyo ilitakiwa iruke kama risasi umbali wa mita 100 kwenda angani.


Anasema ndipo wanajeshi hao waliokuwa wamevaa miavuli walitupwa nje, ambapo mmoja aliyejeruhiwa aliangukia kwenye lami barabarani na aliyekufa alijigonga juu ya paa la  hanga baada ya mwavuli aliokuwa nao kushindwa kufunguka.


Mgawe anasema kuwa kawaida tahadhari zinakuwepo, ila kwa tukio hilo  bado hawajatambua  tatizo lilikuwa ni nini.

No comments:

Post a Comment