Pages


Photobucket

Monday, October 29, 2012

RAIS KIKWETE KUZINDUA UJENZI WA NYUMBA ZA WAHANGA WA MAPOROMOKO NA KIWANDA CHA TANGAWIZI MAMBA MIAMBA LEO.


Rais Jakaya KiweteRais anatarajiwa kuzindua ujenzi wa nyumba Nane za wahanga wa maporomoko ya Ardhi yaliyotokea Novemba 2009 katika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba wilayani Same, Mkoani Kilimanjaro.

Katika Maporomoko hayo watu 24 walipoteza maisha huku Kaya 8 zikikosa mahala pa kuishi baada ya nyumba zao kubomolewa na maporomoko hayo.

Hiyo ni katika utekelezaji wa Ahadi ya Rais Kikwete yaliyotokea Novemba 2009 kujenga nyumba hizo kwa wahanga hao wakati alipowatembelea kuwafariji.
Rais Pia akiwa Mamba Miamba atapata fursa ya kufungua Kiwanda cha Kusindika Tangawizi cha Ushirika wa Walima Tangawizi Mamba Miamba.

Baada ya kufungua nyumba hizo na Kiwanda, Rais Kikwete atahutubia Mkutano wa hadhara na baadae kuelekea Wilaya ya Mwanga na  kuweka jiwe la msingi  hosteli ya wasichana shule ya Dkt. Asha-Rose  Migiro.
 Mmoja wa wafanyakazi wa Kiwanda cha Tangawizi Mamba Miamba, wilayani Same mkoani Kilimanjaro, Omary Kapara akianika Tangawizi iliyokwisha safishwa kabla ya kuanza uzalishaji.
Mbunge wa Same Mashariki, Mh Anne Kilango Malecela akiwa katika maandalizi ya mwisho mho Kimejengwa kwa juhudi zake wisho kabla ya kufunguliwa Kiwanda cha Kusindika Tangawizi ambacho kimejengwa kwa jitihada zake kama Mbunge.

No comments:

Post a Comment