Hali si shwari jijini Dar es salaam maeneo ya katikati ya jiji karibu kabisa na kituo cha polisi cha kati (Centra Police) hivi sasa, baada ya lundo la watu wanaosadikika kuwa ni Waislam wenye Imani kali na kuamua kuzingira kituo hicho kwa lengo la kushinikiza kuachiwa huru kwa katibu wa jumuiya ya kiislamu Sheikh Issa Ponda (Pichani) ambaye alikamatwa jana mida ya saa 4:30 usiku.
Askari ya Polisi wametanda katika eneo hilo huku wakilazimika kutumia mabomu ya machozi na kuwatawanya watu hao ambao wanaonekana kukataa kuondoka mpaka kiongozi wao atakapoachiwa.
Sheikh Issa Ponda ni mmoja kati ya watu 38 wanaoshikiliwa na Polisi kutokana na tuhuma za mbalimbali zikiwemo za uchochezi wa Serikali iliyopo madarakani na kuchochea vurugu za Udini baina ya Waislamu na Wakristo ikiwemo ile iliyotokea hivi karibuni eneo la Mbagala.
*********************************************************************************************************************************************************
*********************************************************************************************************************************************************
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi kanda maalum,Suleiman Kova, alisema
kuwa Ponda amekamatwa kutokana na kukabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo
uchochezi dhidi ya Serikali iliyoko madarakani.
S.H. KOVA -DCP KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUMU YA POLISI DAR ES SALAAM AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO KATIKA KITUO KIKUU CHA POLISI KATI
Makosa
mengine ni uchochezi wa udini kati ya waislamu na wakristo na ndani ya waislamu
wenyewe,kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani jijini.
Tuhuma
nyingine ni kulazimisha watu kufanya maandamano hasa wanawake na watoto,kumtisha
kumuua sheikh Mkuu Mufti Issa Shaaban bin Simba, kujisifia kuingia Makao Makuu
ya Jeshi la Polisi bila ruhusa na uvamizi wa kiwanja.
Tuhuma
nyingine ni kuingilia uhuru wa Mahakama, umwagaji wa damu, uchomaji wa makanisa
zaidi ya nane, uharibifu wa magari, wizi, upotevu wa vifaa vya makanisa.
“Sheikh
ponda amekuwa mstari wa mbele kupambana na vyombo vya dola na kuingilia uhuru
wa Mahakama kwa kudai watuhumiwa waliokamatwa kwa uvunjaji wa makanisa na
kufikishwa Mahakamani waachiwe mara moja kabla ya siku saba”alisema.
Ponda
alikamatwa juzi majira ya saa 4:30 usiku akiwa kwenye pikipiki kuelekea katika
maficho yake maeneo ya Temeke.
“Juzi
usiku sijalala kabisa kuhakikisha oparesheni ya kumkamata inakwenda salama, Ponda
ni mjanja sana ila Serikali ina mkono mrefu kabla ajaingia katika maficho yake
Temeke,alijaribu kukimbia ili atoroke lakini akakamatwa”alisema.
Kova
pia alisema kuwa mnamo Oktoba 12,mwaka huu Ponda aliwaongoza wafuasi wake na
kuvamia kiwanja namba 311/2/4 block T chang’ombe mali ya kampuni ya Agritanza kwa madai ya
kulikomboa.
“Ponda
akiwa na wafuasi wake walivamia kiwanja hicho cha agritanza na kudai kuwa
wanakomboa mali za waislamu zilizouzwa na Bakwata,uchunguzi wa awali unaonyesha
kuwa kiwanja hicho kina hati miliki namba 93773 iliyotolewa na Wizara ya Ardhi
pamoja na mikataba mbalimbali ya kuuziana”alisema
Aidha
Kova alisema kuwa uongozi wa Bakwata ulipeleka mashahidi kuthibitisha uhalali
wa kiwanja hicho na kusema kuwa watu waliovamia wanakabiliwa na shitaka la
kuingia kwa jinai pamoja na uharibifu wa mali.
“kati
ya watu 38 tuliowakamta wanawake ni saba na wanaume ni 31 na tuliwakuta na
silaha mbalimbali kama visu,mapanga,sururu na vifaa vya kuvunjia na vya
ujenzi,jenereta na kujenga jengo la haraka”alisema Kova.
Aidha
Jeshi la Polisi limesema kuwa limemvumilia Ponda kwa muda mrefu na kuwataka
watu wanaoandamana kinyume cha taratib kuacha.
“Nawasifu
sana wakristo ni wavumilivu,wanabusara kwa tukio la mbagala la kuchoma makanisa
la sivyo hali ingekuwa ya hatari na hata hivyo Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu
haijasajiliwa kisheria”alisema.
Kova
amewataka wafuasi wengine wajisalimishe kwani opareheni inaendelea na
watawachukulia hatua za kisheria.
Pia
amewaasa wananchi kutumia akili zao binafsi na kuacha kufuata mkumbo
watashughulikiwa.Jeshi la Polisi linatarajia kumfikisha Mahakamani baada ya
upelelezi kukamilika.
No comments:
Post a Comment