Askofu Michael Henry Hafidhi ( mwenye vazi jekundu) Askofu wa Anglican zanzibar
Akizungumza na shirika la utangazaji BBC kupitia vipindi vyake vinavyorushwa na kituo cha Television ya Star TV (Jana 19/10/2012 saa 3 usiku) Askofu huyo amesema ameamua kuchukua hatua hiyo kutokana na vitisho vilivyo tolewa kwake na kikundi cha Uamsho, kwamba wanahitaji kumkamata kwa sababu kiongozi wao (FARID) ameshikwa kwa hiyo kushikwa kwake kutaishinikiza Serikali iweze kumtoa huyo kiongozi, Hata hivyo Bw.Salim Kikeke (Mtangazaji wa shirika la utangazaji la BBC) alitaka kufahamu uhakika alio nao Askofu huyo kwa kuamini vitisho hivyo vinatoka katika kikundi cha uamsho, Askofu huyo alisema ' Tayari anazo meseji za vitisho (meseji zinazo jitambulisha kuwa wao ni uamsho) katika simu yake ambazo zimetoka katika kundi hilo la uamsho na kuongeza kuwa katika Tovuti yao pia wamebainisha suala hilo ambapo kundi hilo limebainisha kwamba kama sio yeye basi atakamatwa Askofu SHAYO"
Akisisitiza,Askofu huyo amesema lengo la kundi hilo kuwakamata ni kuishinikiza Serikali imuachie kiongozi wao.
Hata hivyo Salim Kikeke alimuuliza Askofu huyo kama tayari amefika katika vyombo vya usalama kufuatia vitisho hivyo.Askofu huyo alisema " tayari tumetoa taarifa na mpaka sasa vyombo vya usalama vinafahamu suala hilo ambapo vyombo hivyo vimesema vitalishughulikia ,ingawa wamesema niandike maelezo na mimi nikaona maelezo ya nini wakati kila kitu kinaonekana" alisema Askofu huyo.
Askofu huyo alipotakiwa kueleza sababu za yeye hasa kwanini anadhani kwamba Kundi la uamsho lingeweza kumdhuru, alisema "kikundi cha uamsho kimekuwa kikitimiza malengo yake ,mfano kilisema kitahitisha mkutano wake ,na mkutano huo ulifanyika,hivyo na sisi tunaogopa na kuwa na hofu kubwa maana uamsho wakifanya kitu wanafanya kweli".Alisema Askofu huyo na kudai kutopewa ulinzi na jeshi la polisi licha ya kutoa taarifa hizo katika vyombo vya usalama.
Kwa upande wake mtangazaji wa Shirika la utangazaji la BBC Bw. Salim Kikeke alisema jana alizungumza na jeshi la polisi kupitia kwa mkurugenzi wa makosa ya jinai DCI Yusuph Ilembo kutoka zanzibar ambalo lilisema halina taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo .
No comments:
Post a Comment