Pages


Photobucket

Wednesday, October 10, 2012

BENKI KUU YA DUNIA YASEMA VIJANA NI RASLIMALI KUU BARANI AFRIKA


Benki Kuu ya dunia inaeleza kwamba kuongezeka bidhaa zinazosafirishwa nchi za nje na kuongezeka mahitaji ya ndani ya bara hili ni mambo yatakayoendelea kuimarisha uchumi wa nchi za Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara kwa miezi iliyobaki ya mwaka huu wa fedha.

Kanda hiyo inatarajiwa kushuhudia ukuwaji wa uchumi wa asili mia 5 nukta 2 kwa mwaka huu wa 2012 na kuendelea hadi mwakani.


Katika mazungumzo kupitia tovuti moja kwa moja, mchumi mkuu wa benkui kuu ya dunia Shanta Devarjan anasema moja kati ya rasilmali kubwa ya Afrika kwa ajili ya ukuwaji wa siku za mbele wa uchumi wake ni idadi ya vijana wanaoingia katika soko la ajira.


 Shanta Devarjan -Mchumi mkuu Banki ya Dunia
 
“Huwenda Afrika ikawa chanzo pekee cha kupatikana vijana hivi karibuni kwa sababu sehemu nyingine za dunia watu wanazeeka na sehemu nyingine ikiwa ni pamoja na ulaya japan na marekani watu wanazeeka kwa kasi sana. Hivyo hili ni jambo kubwa, afrika huwenda ikawa bara lenye nguyvu katika siku za mbele.” Amesema Devarjan.
Lakini Devarajan anasema ukuwaji wa idadi ya watu hasa vijana inaweza kuwa na Baraka na wakati huo huo  kuleta hasara, na ikiwa haikusimamiwa vyema, basi  huwenda ikatishia maendeleo ya uchumi.
“Hatari kubwa kabisa au kitisho kikubwa ni ukweli kwamba licha ya ukuwaji huu idadi ya nafasi za ajira ya uzalishaji zinazobuniwa kutokana na ukuwaji huo ingali ni ndogo sanakulingana na idadi ya vijana wanaoingia katika soko la ajira kila mwaka.”

Benki Kuu ya dunia inasema sekta ya rasilmali asili kote katika bara hilo inaleta matumaini makubwa lakini kuna hatari ya kuwa ni mzigo kwa nchi hizo kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni laana kutokana na rasil mali ambapo mapato kutoka rasilmali asili yanashindwa kuboresha maisha ya raia wa kawaida.

Mchumi mkuu wa benki kuu ya dunia Punam Chuhan-Pole anasema takwimu zinaonesha hii tayari ni hali inayotokea katika nchi zenye utajiri wa rasilmali asili.

“Ukiangalia kiwango cha mapato kinachowafikia watu maskini kabisa ambao ni asili mia ya watu wote ni kidogo mno. Ni kiasi cha asilimia 6 ukilinganisha na kile unachoshuhudia katika nchi zisizo na rasimlai hizo.”
Benki kuu inaeleza kwamba utawala bora ndio msingi mkuu wa kukabiliana na laana hiyo ya rasilmali.

Ushauri huo ni muhimu hasa kufuatia kugunduliwa mafuta huko Kenya, Sierra Leone na Liberia na gesi ghafi kwenye pwani ya Tanzania na Msumbiji.
*****Chanzo cha habari VOA****

No comments:

Post a Comment