Pages


Photobucket

Sunday, October 28, 2012

Manchester yailaza Chelsea 3 - 2


Timu ya Manchester United imeifunga Chelsea katika uwanja wake wa nyumbani wa Stamford Bridge kwa jumla ya magoli 3 - 2 katika mechi iliyochezwa siku ya Jumapili.
Katika mechi hiyo wachezaji wawili wa Chelsea Fenarndo Torres na Branislav Ivanovic walitolewa baada ya kupewa kadi nyekundu na kuwapa nafasi Manchester United kutumia upungufu huo kutawala mchezo.
Katika mechi nyingine iliyochezwa siku ya Jumapili Newcastle imeifunga West Bromwich Albion kwa magoli 2 - 1 , huku Liverpool ikishindwa kulinda magoli yake mawili iliyoyapata kipindi cha kwanza pale ilipocheza na Everton na kutoka sare ya magoli 2 -2.
Mechi nyingine iliyochezwa hapo Jumapili ilikuwa kati ya Tottenham na Southampton ambapo Tottenham ilitoka kifua mbele baada ya kukandamiza Southampton magoli 2 - 1 magoli yaliyofungwa na Gareth Bale na Clint Dempsey.








No comments:

Post a Comment