Pages


Photobucket

Friday, October 19, 2012

RWANDA YAJIUNGA NA BARAZA LA USALAMA UN

                                            RAIS WA RWANDA  PAUL KAGAME 
Rwanda imechaguliwa kuwa mwanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa miaka miwili ijayo
Kura hiyo inakuja siku moja baada ya ripoti ya Umoja wa mataifa kufichuliwa ikisema kuwa nchi hiyo inaunga mkono waasi katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Nchi zitakazoshikilia nafasi tano zisizo za kudumu katika baraza hilo lenye wanachama kumi na tano, ziliamuliwa na umoja wa mataifa hapo jana.
Argentina, Australia, Korea Kusini na Luxembourg pia wameteuliwa kuketi kwenye baraza hilo.
Kulingana na ripoti hiyo ya wataalamu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa na ambayo ilifichuliwa na shirika la habari la Reuters, waziri wa ulinzi wa Rwanda anaongoza kw akutoa amri kwa waasi wa M23 wanaoendeleza uasi Mashariki mwa DRC tangu mwezi Aprili.
Wataalamu pia walishutumu Uganda kwa kuunga mkono waasi.
Rwanda na Uganda, zimekanusha madai hayo.
DRC ilielezea upinzani kuhusu Rwanda kugombea nafasi hiyo lakini mmoja wa wanadiplomasia wa Rwanda alisema kuwa wapiga kura wasingeshawishiwa na ripoti hiyo isiyo na msingi
Rwanda itachukua nafasi hiyo ambayo inashikiliwa na Afrika Kusini mwezi Januari.
Katika taarifa ya waziri wa mambo ya nje Rwanda, Louise Mushikiwabo serikali yake inaweza kutoa mwongozo kuhusu mambo yanayohusiana na vita na amani kwa sababu ya mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini humo ambapo watutsi milini moja waliuawa.

   *********SOURCE: BBC *****

No comments:

Post a Comment