Kiongozi wa kisiasa wa M23 Jean Marie Runinga
Waziri wa ulinzi nchini Rwanda, ametuhumiwa kwa
kuamuru uasi katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Taarifa hizi ni
kwa mujibu wa ripoti ya wataalamu wa Umoja wa mataifa.
Ripoti hiyo ya kisiri, iliyofichuliwa na shirika
la habari la Reuters, inasema kuwa Uganda pia inaunga mkono waasi wa
M23 ambao wamekuwa wakipigana na jeshi la DRC tangu mwezi Aprili.
Ripoti hii inakuja baada ya ripoti
nyingine ya Umoja wa Mataifa kutolewa mwezi Juni ambayo ilituhumu Rwanda
kwa kuunga mkono waasi hao
Lakini Rwanda na Uganda zimekuwa zikikna madai ya kuunga mkono waasi wa M23.
Duru zinasema kuwa katika kipindi cha miongo
miwili iliyopita, Rwanda imeunga mkono makundi ya waasi Mashariki mwa
Congo, kama njia moja ya kupiga vita waasi wa kihutu waliokimbilia eneo
hilo baada ya mauaji ya kimbari mwaka 1994.
Baadhi wanatuhumu Rwanda kwa kutumia waasi
kupigana vita vyake dhidi ya DRC , nchi ambayo ina utajiri mkubwa wa
madini na eneo zima la Maziwa Makuu.
Taarifa za hivi punde za wataalamu wa baraza la
usalama la Umoja wa Mataifa zinatoa maelezo zaidi kuhusu Rwanda
kujihusisha na vita vya DRC.
Maelfu ya watu wameachwa bila makao kufuatia mapigano Mashariki mwa DRC
Wataalamu hao wanasema kuwa waasi wa M23
wanapokea amri za moja kwa moja kutoka kwa mkuu wa majeshi ya Rwanda,
Generali Charles Kayonga, " ambaye naye anafuata amri za waziri wa
ulinzi Generali James Kabarebe.
Wataalamu hao pia wanasema kuwa Rwanda imekuwa
ikitoa silaha kwa waasi hao na kuweka mikakati ya kusajili waasi zaidi
ili kuliganya kundi hilo kuwa kubwa.
Maelfu ya watu nchini DRC wamepoteza makao yao kufuatia vita hivyo kati ya waasi na wanajeshi wa Rwanda.
Ripoti hiyo iliyoonwa na shirika la habari la
Reuters inasema kuwa wanajeshi wa Rwanda na Uganda wamesaidia waasi wa
M23 kupanua harakati zao katika eneo la Mashariki mwa DRC
********Chanzo cha Habari ni BBC*******
No comments:
Post a Comment