Pages


Photobucket

Wednesday, October 17, 2012

MWANAHARAKATI WA MAPENZI YA JINSIA MOJA ALIYEGOMBEA KITI CHA USENETA NCHINI KENYA


Bw. DAVID KURIA MBOTE (Pichani) ni  Mwanaharakati Maarufu nchini kenya ambaye anagombea nafasi ya kiti cha USeneta jimbo la Kiambu nchini Kenya katika uchaguzi ujao. "Najua ni uamuzi mugumu  lakini najipa matumani ya kushinda" Alisema.
Mwanaharakati huyu ambaye anagombea nafasi hiyo, anafahamika bayana na kuweka wazi  kwamba yeye ni moja kati ya watu wanaojihusisha na Mapenzi ya jinsia moja,Suala ambalo ni kinyume na Mila na desturi za Afrika  pamoja na watu wa dini mbalimbali (Waislam na wakristo).
Wachambuzi wa mambo wanamtaja Bw. David kuwa huenda akashindwa katika kinyang'anyiro hicho kutokana na tabia yake ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.Kumekuwepo na tetesi kwamba huenda  anapata misaada ya kifedha  kutoka baadhi ya  nchi za Magharibi ingawa  suala hilo yeye mwenyewe  wakati akiojiwa na Shirika la BBC (Jana ) alikanusha kupata msaada wowote ule kutoka sehemu yoyote Duniani.
Bw. David mwenye umri wa Miaka 38 sasa, ni   kijana Mtanashati  anaonekana kuwashangaza watu wengi barani Afrika ,hususani katika nchi yake ya Kenya  kwa kujihusisha na Mapenzi ya jinsia moja. 

 
Bw. David ambaye  amekuwa akitetea haki za watu wanaojihusisha na Mapenzi ya jinsia moja ,ametaja  vipaumbele vyake kuwa ni pamoja na kuhakikisha analeta mabadiliko  ya kisiasa katika misingi ya utawala bora kwa lengo la kufufua matumaini  kwa masuala ya kijamii katika jimbo lake, Ingawa ameongeza na kusema  atajitahidi   kutunga sheria  za kupambana na ugojwa wa ukimwi. 
Pamoja na mipango mikubwa aliyo nayo  bado atakabiliwa na changamoto kubwa, kwani jamii ya wakenya  hawakubali  Utamaduni wa mapenzi ya jinsia moja.




******Chanzo cha habari ni kutoka nchini kenya kwa msaada wa Mitandao****

No comments:

Post a Comment