Pages

Wednesday, December 3, 2014

WANAFUNZI HAWA NI TISHIO WAPATA GPA 4.9 NI KUTOKA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA CBE


Bw. Peragius  Cosmas mwanafunzi aliyehitimu shahada ya Uhasibu na kupata  GPA 4.91 Akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha CBE Prof.Emanuel Mjema.
Bi. May Issa  mwanafunzi aliyehitimu shahada ya kwanza ya Usimamizi wa manunuzi  na kupata  GPA 4.92 Akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha CBE Prof.Emanuel Mjema.


Kwa kile ambacho kimeonekana ni tishio kwa chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)  wanafunzi hawa  kutoka kampasi ya Dodoma  wameweza kupata ufaulu mkubwa katika masomo yao.

 Bi. May Issa  Mwanafunzi  aliyehitimu shahada yake ya kwanza ya Usimamizi wa  Manunuzi  katika mahafali ya 49 ya chuo cha Elimu ya Biashara CBE Dodoma mwaka 2014 ametangazwa  kuwa mwanafunzi wa kwanza aliyeongoza kwa ufaulu kwa kupata GPA ya  4.92. ambapo  aliweza kupata alama  A  28 , alama  B+ tatu  na  alama  B  moja  kati ya masomo  32  ya shahada yake ya kwanza  ya  Usimamizi wa manunuzi akifuatiwa na  Bw. Peragius Cosmas  aliyepata GPA ya 4.91.

 Kwa upande  wake Mwanafunzi mwingine  Bw, Peragius Cosmas  aliye kuwa akisoma Shahada ya kwanza ya Uhasibu   yeye pia alionyesha maajabu kwa kuweza kupata GPA ya  4.91  ambapo aliweza kupata alama  A  29 na  alama  B+ tatu    kati ya masomo  32  ya shahada yake ya kwanza  ya  uhasibu.

Hivi  karibuni katika Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM)  pia tulishuhudia  Msichana   Doreen Kabuche aki ]ongoza kwa ufaulu UDSM kwa kuwa  Mhitimu bora wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2014, Doreen Kabuche alitangazwa kuwa kinara kwa ufaulu kwa kupata alama A 32 na B+ sita kati ya masomo 38 ya shahada ya Takwimu Bima (Actuarial Science). Kwa alama hizo, Doreen alipata wastani wa alama za ufaulu (GPA) 4.8 na kuacha alama ya 0.2 ili kufikia kiwango cha juu kabisa cha ufaulu cha alama tano, Bi. May  Issa akionekana mwenye furaha siku ya mahafali  ya 49 iliyofanyika hivi karibuni katika chuo cha Elimu ya biashara kampasi  ya Dodoma.

Bw. Peragius Cosmas akionekamna mwenye furaha  katika mahafali ya  49 ya  chuo cha CBE iliyofanyika hivi karibuni katika  Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dodoma.
  Bw. Peragius  Cosmas (kulia)  na May  Issa  (Kushoto) wakiwa na tabasamu  kufurahia kile walichoweza kukivuna katika kipindi chote cha miaka mitatu katika masomo yao CBE Dodoma .
  Rais mstaafu wa Serikali ya Wanafunzi CBE  kampasi ya Dodoma 2013/2014 Bw. Remidius Emmanuel (kulia) akimpongeza  Bi. May  Issa kwa kufanya vizuri katika  masomo yake  kwa kipindi chote cha masomo yake.

Sunday, February 9, 2014

MAAJABU YA DUNIA;HII NDO PICHA YA MAITI ILIYOGANDA NA KUTAA KUZIKWA KWA MDA WA MIAKA 500

Girl Frozen For 500 years
Girl who was killed as an offering to the
Inca gods sometime between 1450 and
1480, at approximately 11–15 years old.
best-preserved mummy ever found, with
internal organs intact, blood still present in
the heart and lungs, and skin and facial
features mostly unscathed. No special
effort had been made to preserve her and
500 years later still looked like sleeping
child
Girl Frozen For 500 years
Girl who was killed as an offering to the
Inca gods sometime between 1450 and
1480, at approximately 11–15 years old.
best-preserved mummy ever found, with
internal organs intact, blood still present in
the heart and lungs, and skin and facial
features mostly unscathed. No special
effort had been made to preserve her and
500 years later still looked like sleeping
child
source- thechoicetz.com

HII NDIO HISTORIA YA MASANJA MKANDAMIZAJI................SOMA HAPA KUJUA ZAIDI


Kwa wapenzi wa sanaa ya vichekesho, jina la Masanja Mkandamizaji si geni masikioni mwao kutokana na uwezo wake wa kuwavunja mbavu watazamaji pale anapoonekana katika runinga na Kundi la Original Comedy.

Licha ya kufika hapo alipo sasa, msanii huyu anakiri wazi kuwa amepitia katika ugumu hususani wakati alipoamua kuanza maisha binafsi ya kujitegemea baada ya kutoka nyumbani kwa dada yake alipokuwa akiishi

Anasema kabla ya kuondoka kwa dada yake alimuomba amtafutie chumba ili ajitegemea na kuanza maisha binafsi kama kijana .

Nilimwambia dada anitafutie chumba na alifanya hivyo ingawa alikuwa anahofia kama nitaweza ,basi nikapata 'geto' langu maeneo ya Tabata Aroma na nilitakiwa kulipa kodi ya Sh5000 kwa mwezi, anasema Masanja.

Anakiri wazi kuwa changamoto katika maisha ndizo zilizochangia kumfikisha mahali alipo sasa kwani licha ya kuwa katika hali ngumu hakukata tama bali alizidi kujituma kwa nguvu zake zote.

Anasema kuna wakati ilikuwa vigumu kuipata hata hiyo hela ya kodi kwahiyo ilikuwa inamlazimu kurudi kwa dada yake kwa muda unapofikia wakati kulipa kodi.

Yaani hiyo Sh5000 kuipata ilikuwa shughuli maana ilikuwa ikifika karibu na mwisho wa mwezi narudi kwa dada kuzuga kidogo ili mama mwenye nyumba ajue nimesafiri,anasema.

Anasema alianza kwa kulala chini mpaka siku alipofanikiwa kupata fedha kidogo iliyomuwezesha kununua godoro la sufi jambo ambalo anajivunia nalo kwani aliweza kununua kwa jasho lake.

Anaongeza kuwa kamwe hawezi kumsahau marehemu Steven Kanumba pamoja na mtu mwingine aliyemtaja aitwaye Mtitu kutokana na mchango wao uliosaidizi kumfikisha hapo alipo sasa .

Namshukuru sana marehemu Kanumba alikuwa anakuja kunichukua kule Tabata tunaenda kupiga 'inshu' ambazo zilikuwa zikiniingizia pesa kidogo iliyoniwezesha kuishi hata hivyo maisha yalikuwa magumu.

Wakati naanza maisha sikuwahi kutoa hela hata ya kununua chipsi kavu lakini siku moja nilifanya kazi na Mtitu ambayo alinilipa laki moja sikuamini macho yangu, kwa mara ya kwanza kununua chipsi kuku kwani nilikuwa nikitamani mlo huo nililazimika kusaidia kumenya viazi kwa washikaji,

Sambamba na uchekeshaji Masanja pia amejiingiza katika shughuli za kumtukuza Mungu baaada ya kuokoa na sasa anafanya vizuri pia katika uimbaji wa nyimbo za injili na kesho Jumapili atazindua albamu yake ya pili ya muziki wa Injili inayoitwa Hakuna jipya chini ya jua.

Saturday, February 1, 2014

CCM YAZIDI KUJIIMARISHA MBEYA MJINI

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akigawa kadi kwa wanachma wapya waliojiunga na CCM baada ya kuzindua shina la Wakereketwa la Madereva wa Bodaboda Inyara,Iyunga mkoani Mbeya.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Inyara, Iyunga mjini mkoani Mbeya baada ya kuzindua shina la wakereketwa ambapo aliwaambia CCM imejiandaa vya kutosha kwa ushindi wa 2015..
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Inyara ,Iyunga baada ya kuzindua shina la wakereketwa la madereva wa Boda Boda.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wafanyabiashara ndogo ndogo wa  Inyara ,Iyunga mkoani Mbeya.

Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Iyunga mara baada ya kufungua shina la wakereketwa ambapo alisisitiza kwa madereva wa boda boda kuwa Umoja ni Ushindi hivyo kukiwa na umoja dhabiti kati yao basi watafanikiwa sana na aliwasihi vijana waepuke dhambi ya kubaguana.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa na dereva wa BodaBoda wa Iyunga Itika Mwangosi ambaye amejiunga na chama cha mainduzi na kukabidhiwa kadi yake na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM Iyunga mara baada ya kufungua shina no.3 la Bodaboda .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na mmoja wa wapenzi wa CCM aliyekuwa akisafiri kwa Bajaj ,Soweto mjini Mbeya.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitembea mitaa ya Soweto kwenda kufungua shina la wakereketwa wauza chakula na wauza matairi kata ya Ruanda,Jumla ya mashina manne yalizinduliwa leo mjini Mbeya.

Friday, January 31, 2014

Chadema kususia Bunge la Katiba

Wakati Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akisema wabunge wa chama chake watasusia vikao vya Bunge Maalumu la Katiba ikiwa hoja ya kuundwa kwa Serikali tatu itapingwa na wabunge wa CCM, Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF), Ismail Jussa Ladhu ametaka kuvunjwa kwa Muungano.
Akihutubia kwenye Uwanja wa Tubuyu nje kidogo ya Mji wa Morogoro juzi, Mbowe alisema wabunge wa chama chake wataandamana nchi nzima kufikisha ujumbe kwa wananchi kwamba maoni yao yamepingwa na wabunge wa CCM walio wengi.
“Tutawaeleza wananchi kwamba maoni ya CCM ndiyo yameonekana ya maana kuliko ya wananchi ambao ni wengi zaidi,” alisema Mbowe kwenye mkutano huo ambao ni sehemu ya Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko - M4C Pamoja Daima.
Alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilikusanya maoni na kubaini kuwa asilimia 62 ya Watanzania wanataka Serikali tatu za Tanganyika, Zanzibar na ya Muungano.
“Serikali ya CCM haitaki kusikia maneno Serikali tatu wanasema sera yao ni ya Serikali mbili, wanafanya kila hila ili kuikataa hoja hiyo. Natangaza kwamba wakifanya hivyo tutasusia na kwenda kuwashtaki kwa wananchi,” alisema Mbowe.
Aliongeza kwamba wataandamana kuanzia Kagera hadi Mtwara kuwaeleza wananchi kwamba hoja yao imepingwa na CCM.
Mbowe alisema baadhi ya viongozi wa CCM wamekuwa wakitoa kashfa dhidi ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kwamba amechukua maoni ya Chadema.
“Wanakosea hayo si maoni ya Chadema, bali ni maoni ya wananchi, Warioba amezingatia maoni ya wananchi,” alisema.
Mwenyekiti huyo alisema Katiba inayotafutwa si ya chama, bali ni ya Watanzania na kwamba inashangaza CCM kuipinga hoja Serikali tatu.
“Tunafahamu wanaogopa kuikubali hoja ya Serikali tatu kwa sababu wanafahamu huo ndiyo utakuwa mwisho wao wa kuwa madarakani,” alisema Mbowe huku akishangiliwa na wafuasi wa chama hicho.
Alisema CCM wanaelewa kwamba kukiwa na Serikali tatu, Chadema kitashinda Tanganyika na CUF Zanzibar katika uchaguzi wowote utakaoitishwa.
“Kwa hiyo hivi sasa wana wasiwasi kweli, wanatafuta kila njia ya kuichakachua hoja ya Serikali tatu lakini wafahamu kuwa Chadema wanaifuatilia hoja hiyo kwa ukaribu,” alisema.
Aliwataka wananchi kufuatilia Bunge Maalumu la Katiba litakapoanza mwezi ujao ili kuangalia wabunge wao wanavyowawalisha katika suala hilo muhimu.
Hata hivyo, Mbowe alisema chama hicho kikishinda katika uchaguzi wa mwaka 2015 hakitahangaika kulipa kisasi kwa kuwachukulia hatua za kisheria viongozi, bali kitajikita kutafuta maendeleo.
“Wasituogope tutasamehe kama alivyosamehe aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela. Hatutalipa kisasi tukiingia Ikulu, kwa sababu hakuna binadamu asiye na makosa. Tutaelekeza nguvu zetu kuwaletea maendeleo Watanzania,” alisema Mbowe.
Jussa na Muungano
Akihutubia mkutano wa kampeni katika Jimbo la Kiembesamaki jana, Jussa alisema hakutakuwa na maendeleo yatakayofikiwa Zanzibar ikiwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hautang’oka.
Jussa ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la CUF, alisema Zanzibar yenye watu milioni 1.5 haiwezi kuwa na tatizo la watu kukosa ajira lakini sera na mipango ya kiuchumi imekuwa ikikwama katika utekelezaji wake kutokana na kukosa mamlaka kamili.
Alisema Zanzibar haiwezi kukopa katika taasisi za kimataifa bila ya kuwekewa dhamana na Waziri wa Fedha wa Muungano wakati Zanzibar ni nchi na kuwataka wananchi kutumia kura zao katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kuleta mabadiliko ya kiutawala.
“Hakuna sababu ya vijana Zanzibar kukosa ajira, kuna watu wasiozidi milioni 1.5, Muungano umefika wakati ung’oke, ndiyo kikwazo cha maendeleo ya Zanzibar na watu wake kiuchumi na kisiasa,” alisema Jussa.
Alisema mradi wowote unaobuniwa Zanzibar hauwezi kupata mfadhili bila kuwekewa dhamana na Serikali ya Muungano na kukwama kwa juhudi zote za kujiunga na jumuiya za kimataifa akitolea mfano Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu (OIC).
Alisema Rais wa Zanzibar amepoteza mambo muhimu chini ya mfumo wa Muungano ikiwa ni pamoja na kutopigiwa mizinga 21 akiwa nje ya nchi, kupeperusha bendera ya Zanzibar, kutokagua gwaride na kupigiwa wimbo wa Taifa la Zanzibar.
“Haya ya sasa si mamlaka kamili, wapi Dk Shein alikokwenda akapigiwa mizinga 21 au alipeperushwa wapi bendera ya Zanzibar wakati wa safari zake za nje?” alihoji Jussa.

FIRST MEETING OF THE AFRICAN AMBASSADORS IN THE AFRICA HOUSE

 Balozi wa African Union nchini Marekani Mhe. Amina Salum Ali (kulia) akiongoza mkutano wa kwanza wa Mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Marekani kwenye jengo jipya la ofisi ya African Union lililopo Georgetown, Washington, DC. siku ya Jumatano January 29, 2014
 Waheshimiwa Mabalozi waliohudhuria mkutano huo wa kwanza wa Mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Marekani kwenye jengo jipya la ofisi ya African Union lililopo Georgetown, Washington, DC. siku ya Jumatano January 29, 2014.

 Waheshimiwa mabalozi wakifuatilia mkutano wa kwanza wa Mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Marekani kwenye jengo jipya la ofisi ya African Union lililopo Georgetown, Washington, DC. siku ya Jumatano January 29, 2014

D’BANJ NA YAYA TOURE WAUNGA MKONO KAMPENI YA KILIMO YA RAIS KIKWETE

page
D’Banj alishirikiana na washirika wa Kilimo wa Afrika katika uzinduzi wa kampeni ya ‘Shiriki Kilimo’ (Do Agric) kwenye kongamano la Umoja wa Afrika. Kampeni hiyo inalenga kuwasaidia watu zaidi ya milioni 85 barani Afrika kutoka katika lindi la umasikini kupitia uwekezaji maalumu katika kilimo na sera za kilimo za Maputo zilizoboreshwa.
D’Banj alikuwa mmoja wa waliozungumza Addis Ababa jana wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo yenye lengo la kuwahamasisha viongozi wa kisiasa kutumia sera nzuri zitakazonyanyua uzalishaji, kuongeza kipato na kuondoa mamilioni ya Waafrika kutoka katika umasikini.
“Nataka Waafrika kufahamu kilimo ni msingi mzuri wa uchumi ambacho kinatakiwa kutiliwa mkazo na kuleta mabadiliko katika uchumi wa wananchi na nchi na pia tukitilia mkazo tunaweza kuilisha dunia nzima kwa ujumla sisi kama Waafrika,” alisema D’Banj.
Kwa upande wake mchezaji wa timu ya Manchester City, Toure alisema wakati viongozi wengine wa Kiafrika wakitoa kauli zenye nia njema, kwa sasa ni nchi 8 tu zililizotimiza ahadi zake za kuwekeza 10% ya bajeti za nchi katika kilimo.
“Kwahiyo ni muhimu kufanya zaidi na kwenda mbele zaidi. Kilimo sio muhimu pekee, pia ni lazima. Kilimo kinalipa,” alisemaToure.
Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na asasi mbalimbali za kiraia zikiwemo Pan African Farmers Association (PAFO), Action Aid International , Acord International, Oxfam na Alliance for Green Revolution In Africa (AGRA) mbali na asasi hizo mwanasoka wa kimataifa wa Ivory Coast Yaya Toure pia ametia saini kuunga mkono uhamasishaji huo.
Source:Habari leo