Pages


Photobucket

Wednesday, October 31, 2012

MKUU WA MKOA ARUSHA AAMURU WANAFUNZI WASWEKWE MAHABUSU

 
Picture
Mwanafunzi wa Sekondari ya Kimnyaki, Arumeru, Ezekiel Memiri, alivyoshikiliwa na Askari Polisi Peter Mvula, Mkuu wa Operesheni wa Mkoa baada baada kuamuru akamatwe kwa kosa la kushinikiza maandamano ya Wanafunzi wenzake hadi Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa.
Picture
Mkuu wa Mkoa, Magesa Mulongo akiongea na wanafunzi na kutoa onyo kali kwa wanafunzi ambao hawatarudi shuleni watafukuzwa mara moja
Habari imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya Pamela Mollel

MKUU wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amewasweka lumande wanafunzi watatu wa Shule ya Sekondari Kimnyaki kwa kosa la kushinikiza maandamano ya wanafunzi wenzake hadi Ofisini kwake.

Wanafunzo hao waliokamatwa kwa kosa la kuchochochea maandamano hayo ni pamoja na Ezekiel Memiri, Losijaki Lunde, na Meshack Lomunyaki.

Maandamano ya wanafunzi hao yalikuwa na lengo la kumshinikiza Mkuu huyo wa Mkoa kumuondoa Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo.

Akizungumza na Wanafunzi wa Shule hiyo jana Ofisini kwake alisema kwamba wanafunzi hao wameshindwa kufuata maagizo yaliyoandikwa katika fomu zao za kujiunga na masomo shuleni hapo.

 Mkuu wa Mkoa alisema kwamba ni makosa makubwa kwa wanafunzi kukaidi ama kushindwa kufuata maagizo ya shule hasa yaliyoandikwa katika fomu zao za kujiunga na shule.

“Askari kamata hawa jamaa weka ndani hawana heshima hata kidogo,haiwezekani wakalifanya jiji la Arusha kama kiwanja cha michezo kwamba kila anayehitaji kucheza anaruhusiwa kufika, haya mambo hayawezekani hata kidogo, lazima utaratibu ufuatwe na kila mmoja apewe haki ya kusikilizwa”alisema Mkuu wa Mkoa na kuongeza:

“Tena nataka kuchukuwa nafasi hii kupiga marufuku maandamano yote ya wanafunzi katika Jijini la Arusha, siwezi kukubaliana na suala hili hata kidogo, kuna viongozi wa serikali wapo shuleni,nyinyi mko huku,Mkuu wa Wilaya ya Arumeru yuko huko tayari kwa ajili ya kuwasiliza mmekimbilia kwa Mkuu wa Mkoa tena bila vibali vya maandamano”

 Awali kabla ya wanafunzi hao kufika Ofisini kwake walikutana na vikwazo vya Askari wa Jeshi la Polisi na kuwapiga mabomu ya machozi wanafunzi hao.

Maandamano hayo  yaliyoanza juzi kwa lengo la kumshinikiza Mwalimu Mkuu wa shule hiyo aondolewe kwa kile walichodai kwamba anachangia kudidimiza maendeleo yao kitaaluma na kwamba anafurahia matokeo mabaya ya wanafunzi hao baada ya mitihani yao.

Baada ya Jeshi la Polisi kufanikiwa kuzuia maandamano hayo siku ya kwanza, jana wanafunzi hao walibuni njia nyingine ya kuandamana na kufanikiwa kufika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

“Juzi Mkuu wa Wilaya ya Arumeru alifikia shuleni kwetu akatuambia kwamba angekuja kesho (yaani leo) tukamsubiri hadi saa nne bila mafanikio ndipo tulipobuni njia nyingine ya kuandamana, tukaamua kuondoka shule mmoja mmoja mpaka katikati ya mji, na tulipokutana na askari hao tukaanza tena kupambana na kila walipoturushia mabomu ya machozi sisi tuaanza kuwarushia mawe huku tukinawa usoni”alisema Ezekiel Memiri.
Picture
Wanafunzi wakiwa wamenyanyua juu mabango yenye ujumbe wa kutomtaka mkuu wa shule
Picture

No comments:

Post a Comment