Waziri wa nchi za kigeni wa Marekani Hillary Clinton
amesema kuwa yeye ndiye aliyekuwa na jukumu la ulinzi katika ubalozi wa
Marekani nchini Libya ambapo balozi wake aliuawa mwezi uliopita.
Mauaji ya balozi huyo Christopher Stevens pamoja
na wamarekani wengine watatu limekuwa suala gumu sana katika siku hizi
za mwisho za kampeini za uchaguzi wa urais.
Kamati maalum ya Congress imearifiwa kuwa ombi la kutaka kuongezewa uslama katika ubalozi huo lilikataliwa na idara ya serikali.
Bi Clinton aliambia vyombo vya habari nchini
Marekani kuwa kuhakikisha usalama wa ubalozi wa Marekani kote duniani ni
wajibu wake na wala sio wajibu wa Ikulu ya White house.
Tulichohitajika kufanya katika idara ya mambo ya
ndani ilikuwa kuangazia kilichokuwa kinatokea wala sio kuhusu nini
kitatokea, Bi Clinton aliambia waandishi wa habari.
''Na hilo ndilo nilikuwa naangazia usiku na
mchana kujaribu kuhakikisha kuwa tunajaribu kudhibiti hali kwa
ushirikiano na idara zengine za serikali.'' alisema Clinton
Serikali ya Rais Obama imekuwa ikikosolewa sana
kuhusiana na shambulizi hilo dhidi ya ubalozi wa Benghazi hasa wakati
huu ambapo kampeini za uchaguzi zinaposhika kasi.
***Chanzo cha habari BBC***
No comments:
Post a Comment