Pages


Photobucket

Saturday, June 1, 2013

MUSHARAF AKAMATWA TENA.




ISLAMABAD-PAKISTAN,
Polisi nchini Pakistan wamemkamata rais wa zamani wa nchi hiyo Pervez Musharraf, kutokana na agizo la Mahakama siku ya Alhamisi.

Hatua ya kukamatwa kwa Musharraf ilitolewa na Mahakama hiyo kutokana na uamuzi wake wa kuagiza kifungo cha nyumbani kwa Majaji nchini humo mwaka 2007 akiwemo Jaji Mkuu.

Musharraf, alikamatwa nyumbani kwake nje kidogo ya mji wa Islamabad siku ya Ijumaa na kufikishwa Mahakamani huku serikali ikisema nyumba yake itakuwa jela kwa mujibu wa sheria ya nchi hiyo.

Kiongozi huyo wa zamani wa kijeshi ameonekana siku ya Ijumaa akisindikizwa na polisi Mahakamani na tayari anazuiliwa rumande kwa siku mbili kabla ya kupewa kifungo cha nyumbani.

Hii ni ndio mara ya kwanza kwa Mahakama nchini humo kutoa agizo la kukamatwa kwa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo ambaye pia alikuwa Mkuu wa Majeshi.

Wakati uo huo, Mahakama mjini Islamabad imeanza kusikiliza kesi ya uhaini dhidi ya Musharraf kwa kuagiza kuwepo kwa sheria ya hatari nchini humo mwaka 2007 na ikiwa atapatikana na kosa atahukumiwa kifo au kufungwa maisha jela.

Kiongozi huyo wa zamani pia anatuhumiwa kupanga mauaji ya kiongozi wa upinzani Benazir Bhutto mwaka 2007.

Musharraf mwenye umri wa miaka 69 alikuwa rais wa kumi wa nchi hiyo kati ya mwaka 2001 hadi 2008 kabla ya kujiuzulu na kukimbilia ukimbozini jijini London nchini Uingereza.

Musharraf alirudi nyumbani mwezi uliopita kutoka Dubai alikokuwa anaishi, na kusema kuwa amerudi nyumbani ili kuikoa Pakistan hatua iliyokaatiliwa na tume ya uchaguzi nchini humo.

No comments:

Post a Comment