Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Mh Joshua Nassari alikanusha 
taarifa zilizoandikwa na magazeti ya Uhuru na Habari jana kuwajuzi 
alifyatua risasi na kuzua tafrani katika uchaguzi wa kumtafuta Diwani wa
 Kata ya Daraja Mbili ya Jijini Arusha, uchaguzi uliofanyika juzi ambapo
 mgombea wa Chadema aliibuka mshindi.
Nassari ameyasema hayo jana  
jioni wakati akihutubia katika Mkutano wa hadhara kuzindua kampeni 
nyingine za chama chake kwa ajili ya chaguzi za Serikali za Mitaa kwa 
ajili ya Halmashauri ndogo ya Mji wa Usa River unaotarajiwa kufanyika 
Jumapili ijayo ya Novemba 4, 2012.
Mkutano huo ambao ulihudhuriwa
 na watu wengi, ulifanyika katika viwanja vya Ngaresero Usa-River ambapo
 mbali na Nassari, Katibu wa CHADEMA Kinondoni Ng Henry Kileo nae 
alikuwepo na alipewa nafasi ya kuzungumza.
Nassari alidai kuwa 
katika uchaguzi wa juzi yeye alikuwa Wakala Mkuu wa CHADEMA Kata ya 
Bangata na hivyo kumhusiha na ya Daraja Mbili haelewi inakujaje. Amedai 
kuwa mtu aliyefyatua risasi ni Mwenyekiti wa UVCCM, Godwin Mwalusamba na
 kwamba Polisi walimuweka ndani na kuandika maelezo yake, lakini 
anashangaa kuambiwa ni yeye wakati siyo!
Akifafanua zaidi 
aliviomba vyombo vya usalama avinavyohusika na masuala ya vibali vya 
kumiliki silaha za moto, kufanya uchunguzi wao na waeleze hiyo bunduki 
walimpa lini na ni risasi zimetumika, na kwamba kama ni kumkamata yeye 
yupo huru muda wowote wanaweza kumkamata.
 Mh Nassari akihutubia mkutanoni hapo jana
Mh Nassari akihutubia mkutanoni hapo jana  
 Sehemu ya umati ulijitokeza katika ufunguzi huo uliofanyika katika uwanja wa Ngaresero, Usa-River
Sehemu ya umati ulijitokeza katika ufunguzi huo uliofanyika katika uwanja wa Ngaresero, Usa-River 
 Katibu
 wa CHADEMA Kinondoni, Dar es Salaam, Henry Kileo akizungumza na 
wananchi wa Usa River leo jioni.Nassari alisema kampeni hizo 
zitahitimishwa Novemba 3, 2012 katika viwanja hivyo na kuna uwezekanao 
Mh Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Chama hicho taifa akahudhuria.
 Awanadi wagombea wa Chadema

 Mh
 Nassari aliweza kuwatambulisha rasmi wagombea wa Chama chake 
(waliosimama) watakaoshiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 9 
katika Halmashaur ya Mji Mdogo wa Usa River, uchaguzi unaotarajiwa 
kufanyika Jumapili ya Novemba 4, 2012. Katika wagombea hao, mwanamke 
aliyejitokeza ni mmoja tu, Verian Mushi ambae anagombea mtaa wa 
Magadini.

Wagombea wa Chadema na Mitaa wanayogombania ni hawa wafuatao
1. Verian Mushi – Magadini,
 2. Henry Benjamin Mpinga – Manayata
 3. Ernest Makalla Shilla – Magadirisho
 4. Exaud Jackson Mbise – Nganana
 5. Richard Mohamed Ngungu – Kisambare
 6. Malisa – Mji Mwema
 7. Santrumini Filipo – Mlima Sioni (Lake tatu)
 8. Frank Anael Msuya – Usa Madukani
 9. William – Ngarasero
 
 Baadhi ya viongozi wa Chadema Usa River na wagombea wao
Baadhi ya viongozi wa Chadema Usa River na wagombea wao 
Nassari azungumzia mafanikio ndani ya miezi 5 ya ubunge wake
Katika
 hotuba yake, Mh Nassari aliweza pia kuzungumzia baadhi ya mambo ambayo 
amekwishayafanya kwa wananchi wake wa Arumeru tangu wamchague kuwa 
mbunge wao, takribani miezi mitano iliyopita.
Akiorodhesha mambo 
hayao harakaharaka, Nassari alisema kwamba amekwishakamilisha mradi wa 
majai ya kisima wenye thamani ya sh mil 60 kwa maeneo ya Ngobobo na 
Ngarenanyuki.
Akaeleza kuwa ameanzisha ligi ya mpira wa miguu kwa
 Kata zote za Jimbo lake ambapo amedai kuwa vifaa vimemgharimu zaidi ya 
sh milioni 5. Ligi hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 10 Novemba,
 2012.
Alidai kuwa ameshiriki kwenye harambee nyingi za maji na 
kwamba ya karibuni amechagia kiasi cha sh milion 1.5, pia amechangia sh 
milioni 1 kwaya ya Jimboni kwake iliyomwaomba kuwasaidia.
Mambo 
mengine ni pamoja kusambaza vitabu vyenye thamani ya sh milion 38 kwa 
shule 15 za Kata, sehemu kubwa ikiwa ni msaada wa rafiki zake wa 
Marekani. Pia nmatengenezo ya choo kwa shule ya msingi Liganga, 
kuchangia vikundi vya kina mama.
CHANZO;  NOISE OF SILENCE BLOG