Rais
wa Marekani,Barack Obama akiwahutubia wananchi wa Marekani mara baada
ya kutangazwa ni mshindi katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo,dhidi ya
Mpinzani wake,Mitt Romney.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
ameeleza furaha na shangwe yake kufuatia ushindi wa jana, Jumanne,
Novemba 6, 2012 wa Rais Barack Obama wa Marekani katika Uchaguzi Mkuu wa
nchi hiyo.
Katika salamu zake za pongezi kwa kiongozi huyo wa Marekani ambaye
amechaguliwa tena na wananchi wa nchi hiyo kwa kipindi cha pili, Rais
Kikwete amesema mapema leo, Jumatano, Novemba 7, 2012:
“Nimepokea
kwa furaha na shangwe habari za kuchaguliwa tena kwako kuwa Rais wa
Marekani kwa kipindi cha pili. Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa hakika, kwa niaba yangu
mwenyewe, napenda kukutumia wewe na kupitia kwako Chama cha Democratic
pongezi nyingi kwa ushindi wako wa maana sana.”
Ameongeza
Rais kikwete katika salamu zake hizo: “Kuchaguliwa kwako tena kuendelea
kuongoza nchi yako muhimu na wananchi wake, ni ishara ya wazi ya
uaminifu na imani ambayo wananchi wa Marekani wanayo katika uongozi wako
wa mfano.”
Amesisitiza
Rais Kikwete: “Wakati unajiandaa kuchukua tena uongozi wa nchi hiyo
katika kipindi chako kipya, napenda kukuhakikishia msimamo wangu binafsi
na ule wa Serikali yangu kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa karibu
kabisa na wewe na Serikali yako ya kutukuka, ili kuendeleza uhusiano
bora ulioko kati ya nchi zetu mbili ndugu.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
7 Novemba, 2012
No comments:
Post a Comment