KUTOKA KWA WANAFUNZI WA TANZANIA NCHINI URUSI.
Sisi wanafunzi wa kitanzania nchini Urusi ,tunakosa huduma za 
msingi kama vile malazi , chakula na bima ya afya. Serikali kupitia bodi
 ya mikopo ya elimu ya juu na Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi 
,kwania njema iliamua kusomesha wanafunzi wa kitanzania katika nchi 
mbalimbali duniani ikiwemo Urusi.
Lakini kutokana na utendaji mbovu na ubinafsi wa baadhi ya watendaji wa 
Bodi ya mikopo, kumekua na ucheleweshwaji wa ulipaji wa pesa za kujikimu
 , malazi na bima ya afya kwa zaidi ya miezi mitatu sasa bila sababu za 
msingi toka kuanza kwa mwaka wa masomo 2012/13.
Hali hii imetupelekea wanafunzi kuanza kufukuzwa katika 
hosteli tunazoishi pamoja na kutopatiwa huduma za afya pindi 
tunapo ugua.Ikumbukwe kuwa katika nchi za ulaya huwezi pata matibabu 
kama huna bima ya afya.
Shukrani zetu za dhati ziende kwa Ubalozi wa Tanzania nchi Urusi 
kwa kushirikiana bega kwa bega na Wanafunzi katika kutafuta ufumbuzi 
wa tatizo hili linalotukabili katika kipindi hiki kigumu pamoja na 
majuku mengi waliyonayo, pamoja na jitihada hizo mpaka sasa hakuna 
ufumbuzi wowote uliopatikana.
Tunaandika waraka huu kwa huzuni na masikitiko makubwa sana kwa 
sababu kutopatiwa mikopo mpaka sasa sio tu kunafanya wanafunzi waishi 
maisha magumu na hatari, vilevile kunatia aibu Taifa kwa kutolipa ada 
kwa wakati.
Tunaamini kabisa Serikali kupitia bodi ya mikopo ,wizara ya elimu na mafunzo stadi na ufundi na ubalozi wa Tanzania Nchini Urusi una nia njema kabisa kusomesha vijana wake nje ya nchi, ispokua tu kuna baadhi
ya watendaji wa bodi ya mikopo wamekua wazembe na kutowajibika 
kwani wamekua wakitoa majibu ya uongo na jeuri kwa uongozi wa wanafunzi 
na maafisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Urusi.
Ombi letu kwenu ni kutufikishia ujumbe huu kwa wahusika na watendaji wa 
ngazi za juu za bodi ili waweze kutusaidia sisi wanafunzi wa Urusi ambao
 tupo hatarini huku ugenini.
Tunatumaini kutokana na Uzito wa tatizo letu wahusika watalishughurikia 
na kulitatua tatizo hili kwa haraka zaidi na kutupa ufafanuzi wa 
ucheleweshwaji wa mikopo ya wanafunzi kwa zaidi ya miezi mitatu(3). 
 
 

No comments:
Post a Comment