Akiongea muda mfupi baada ya kuteuliwa, Bi. Ellinah Wamukoya amesema uamuzi huo heshima kwa kina mama.
Kutawazwa kwake kumejiri huku kanisa la 
Kianglikana, likitarajiwa kujadili ikiwa kina mama wataruhusiwa 
kuapishwa kuwa maaskofu wa kanisa hilo.
Askofu wa jimbo la Capte Town, nchini Afrika 
Kusini, amesema kuwa wamechukua uamuzi huo ili wawe mfano kwa wengine na
 pia kuwatakia, viongozi wa kanisa hilo, faraja na hekima ili kujadilia 
sauala hilo kwa haraka.
Kwa mujibu wa ripoti aliyotuma kwa vyombo vya 
habari, askofu huyo wa jimbo la Cape Town, Revd. Thabo Makgoba, amesema 
wimbi kwa sasa linavuma na kuwa wameshuhudia tukio la kihistoria ambao 
ni sawa na bingu kufunguka.
David Dinkebogile aliongoza sherehe hizo na 
kukariri kuwa nia yao kuwa ilikuwa kumuapisha askofu na wale sio mtu 
mweusi, muafrika na raia wa Swaziland.
Askofu Wamukoya ni meya wa zamani wa mji mkuu wa Swaziland Manzini.
Chanzo:BBC Swahili 
 
 


No comments:
Post a Comment