CHAMA Cha 
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinatarajia kuzindua mafunzo ya 
operesheni ya vurguvugu la mabadiliko (M4C) yatakayoanza Novemba 22 
mwaka huu hadi Novemba 23 katika Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera. Mafunzo
 hayo yatatolewa kwa wenyeviti  na makatibu wa vyama hivyo ngazi ya 
wilaya hadi mkoa yenye lengo la kuleta uongozi bora na kueneza sera 
sahihi ya chama hicho. Akizungumza
 na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mafunzo
 na Oganaizesheni, Benson Kigaila alisema mafunzo hayo yamekuwa 
wakifanywa kwa wanachama wao ili kupata mbinu mbalimbali ya kudai haki 
na uwajibikaji wa viongozi na wananchi. “Lengo
 la kutoa mafunzo kwa wenyeviti na makatibu wa vyama vyetu ni pamoja na 
kuwajengea uwezo wa uwajibikaji, kudai haki zao ili kuleta hamasa kwa 
Watanzania kushiriki kikamilifu kwenye mchakato wa mabadiliko, jambo 
ambalo linaweza kuwapa matumaini ya maisha,”alisema Kigaila. Aliongeza
 kutokana na hali hiyo wanaamini kuwa, mabadiliko hayo yataweza kuleta 
uhuru wa kweli na kubadili mfumo wa kiutawala, jambo ambalo litaweza 
kuonyesha mafanikio. Alisema
 kutokana na hali hiyo, jumla ya watu 64 watashiriki kwenye mafunzo hayo
 yakiwamo ya darasani na vitendo ili wajumbe hao waweze kusambaza elimu 
hiyo kwa wananchi katika vijiji na vitongoji,jambo ambalo litaweza 
kurahisisha ufanyikaji wa mikutano ya hadhara. Alisema
 mbali na mafunzo hayo, kutakuwa na mikutano ya hadhara itakayotoa 
mwongozo kwa viongozi hao kuonyesha uelewa wao katika mafunzo hayo, 
jambo ambalo wanaamini wanaweza kufanikiwa. Kwa
 mujibu wa Kigaila, Chadema inatarajia kufanya operesheni ya M4C katika 
mikoa 32 na kwamba operesheni hiyo itakuwa kubwa zaidi ikilinganishwa na
 zilizowahi kufanyika nchini kwa sababu tayari baadhi ya wajumbe 
watakuwa na elimu ya kutosha kuhusu zoezi hilo. 
Mwananchi
 
 


No comments:
Post a Comment