Anayeongoza katika orodha hiyo ni Bakhressa anayemiliki mali na fedha 
zenye thamani ya Dola za Marekani 620 milioni sawa na Sh992 bilioni 
(Dola moja Sh1,600) akifuatiwa na Dewji ambaye utajiri wake ni Dola 560 
milioni (Sh896 bilioni). 
Wengine na kiasi cha mali na fedha wanazomiliki kwenye mabano ni Rostam 
(Sh672 bilioni- Dola 420 milioni) Mengi (Sh448bilioni- Dola 280 milioni)
 na Mufuruki (Sh176 bilioni - Dola 110 milioni).

Reginald Mengi 
WAFANYABIASHARA watano, Said Bakhressa Gulam Dewji, Rostam Aziz, 
Reginald Mengi na Ali Mufuruki, wametajwa na Jarida la Ventures Africa 
linalozungumzia masuala mbalimbali ya uchumi wa Afrika kuwa ndiyo 
matajiri zaidi nchini.
Anayeongoza katika orodha hiyo ni Bakhressa anayemiliki mali na fedha 
zenye thamani ya Dola za Marekani 620 milioni sawa na Sh992 bilioni 
(Dola moja Sh1,600) akifuatiwa na Dewji ambaye utajiri wake ni Dola 560 
milioni (Sh896 bilioni). Wengine na kiasi cha mali na fedha wanazomiliki
 kwenye mabano ni Rostam (Sh672 bilioni- Dola 420 milioni) Mengi 
(Sh448bilioni- Dola 280 milioni) na Mufuruki (Sh176 bilioni - Dola 110 
milioni).
Matajiri hao wamepatikana baada ya kuangalia nafasi zao kifedha, ufanisi
 wa kampuni zao katika soko la hisa, mfumo wa wanahisa katika soko la 
hisa na mtiririko mzima wa fedha katika akaunti zao kwenye benki 
mbalimbali.
Jarida hilo linalotoka mara moja kwa mwezi kutoka Afrika Magharibi, 
limesema matajiri hao wa Tanzania ni kati ya Waafrika wenye utajiri 
ambao ni mabilionea 4,800 kutoka mataifa 17.
Asilimia kubwa ya watu 1,523 ni mamilionea na wamo katika ripoti ya watu matajiri Afrika.
Jarida hilo linataja jinsi matajiri hao walivyokuwa wajasiriamali wadogo kabla ya kuibuka na kuwa mabilionea.
Said Salim Bakhresa
Jarida hilo limesema chanzo cha utajiri wa Bakhressa ni mapato 
yanayotokanana uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwenye viwanda vyake.
Mfanyabiashara huyo aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 na kuanzisha
 biashara zake. Alianza kuuza urojo Zanzibar na baadaye alifungua 
mgahawa miaka ya 1970.
Mgahawa huo ulipanuka na alitumia faida yake kufungua mashine ya kusaga 
pamoja kiwanda za usindikaji vyakula, huku akiunda Kundi la Makampuni ya
 Bakhressa.
Aliendelea kusindika vyakula mbalimbali na kutengeneza unga wa mahindi 
na baadaye kuanzisha kiwanda cha kuoka mikate na baadaye kutengeneza 
chocolate, ice cream, vinywaji na makasha ya kufungashia bidhaa. 
Kutokana na shughuli hizo, kwa mwaka huingiza Sh800 milioni.
Kampuni zake kwa sasa zinafanya biashara mbalimbail katika nchi za 
Tanzania, Uganda, Malawi, Rwanda na Msumbiji na ameajiri zaidi ya 
wafanyakazi 2,000.
Gulam Dewji
Mfanyabiashara huyo ana utajiri unaokadiriwa kufikia Dola 560 milioni kutokana na kuzalisha bidhaa na kutoa huduma mbalimbali.
Ni mmoja wa mataikuni wa Tanzania tangu miaka ya 1970 na kazi yake kubwa ilikuwa kuingiza bidhaa mbalimbali kutoka nje.
Alianza na kampuni ndogo aliyoiita Mohammed Enterprises Tanzania, ambayo
 kwa sasa ni kati ya kampuni kubwa Afrika Mashariki na Kati.
Miongoni mwa mali zake ni Kiwanda cha 21st Century Textiles, moja ya 
viwanda vikubwa vya nguo Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kampuni yake ina 
viwanda vinne, Tanzania na Msumbiji huku ikizalisha Dola 100 milioni kwa
 mwaka. Pia kampuni hiyo husindika juisi kwa matunda ya Tanzania, mafuta
 ya kula, sabuni na tishu.
Kampuni hiyo pia inamiliki kampuni ya bima, makontena, kampuni za kuuza 
mafuta ya petroli na maduka ya kuuza bidhaa mbalimbali zaidi ya 100 
Tanzania nzima.
Hata hivyo, Gulam alisema jana kwamba takwimu zilizotolewa zimekosewa. 
Alisema kwa sasa yuko nje ya Dar es Salaam na atatoa taarifa sahihi 
atakaporejea.
“Kuna baadhi ya tarakimu zimekosewa niko Morogoro kuangalia biashara zangu nikirudi Dar es Salaam nitazungumza,” alisema Dewji.
Rostam Aziz
Ameelezwa kuwa utajiri wake umetokana na kuendesha shughuli zake 
mbalimbali ikiwamo kampuni za mawasiliano ya simu, madini na biashara za
 usafiri wa meli.
Mwanasiasa huyo mwenye asili ya Asia, alichaguliwa kwa mara ya kwanza 
kuwa Mbunge wa Igunga mwaka 1993 na alishinda kwa vipindi viwili.
Aliachana na ulingo wa siasa mwaka 2011. Anamiliki asilimia 19 ya Hisa 
za Kampuni ya Vodacom ambayo ina wateja zaidi ya milioni nane.
Ameelezwa pia kuwa anamiliki Kampuni ya Ujenzi ya Caspian na sehemu ya 
Bandari ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Kampuni ya Hutchison 
Whampoa ya Hong Kong.
Akizungumzia utafiti huo, alisema: “Umefanyika kwa umakini isipokuwa tu 
kwa upande wangu wanasemas ninamiliki asilimia 19 ya Kampuni ya Vodacom 
kitu ambacho si sawa kwani ninamiliki asilimia 35.”
Reginald Mengi
Mengi anakimiliki kampuni mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari, viwanda 
vinavyozalisha vinywaji baridi vya Coca-Cola na ana mgodi wa dhahabu.
Mfanyabiashara huyo baada ya kufanya kazi ya uhasibu ambayo ndiyo 
taaluma yake, alifanya biashara ya kutengeneza kalamu za wino zilizopata
 soko kubwa Afrika Mashariki.
Leo hii, IPP Group ambayo Mengi ni mwenyekiti wake, inamiliki magazeti 
mbalimbali ikiwemo Financial Times, ThisDay na The Guardian, televisheni
 mbili kubwa Afrika Mashariki na Kati EATV na ITV na vituo vya redio. 
Anamiliki Kampuni za IPP Gold na Handeni Gold.
Ali Mufuruki
Utajiri wake unatokana na biashara mbalimbali za rejareja na za ushirika.
Ni mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa Tanzania Infotech Investment Group.
Kampuni hiyo inajumuisha Watanzania na Waganda kwa ajili ya kuuza bidhaa za Afrika Kusini za Woolworth.
 
 

No comments:
Post a Comment