| 
 Kaburi baada ya kuzikwa marehemu 
 
 
Mkazi wa  Swaya jijini Mbeya Ndugu Ndele  Julius amemuua mama yake mzazi
 kwa kumpiga mateke na ngumi kisha kutoroka pasipo julikana Novemba 25 
mwaka huu. 
Tukio hilo limetokea majira ya saa 10 jioni nyumbani kwa mama huyo mara 
baada ya kutokea kwa ugomvi kati ya mtoto wake na kijana  mwingine hali 
iliyopelekea mama huyo kuingilia ndipo alipo kutwa na mauti huo. 
 
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi  Mkoani humo Ndugu Diwani 
Athumani amesema kuwa Chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliokuwepo kati ya
 mtoto wake na kijana  mwenzake kitendo ambacho kilipelekea mama huyo 
kuingilia ugomvi huo . 
 
Amesema wakati  mama huyo akijaribu kuamulia ugomvu huo mtoto wake 
alicha kupigana na mwenzake na kuanza kumshambulia mama yake kwa kumpiga
 ngumi na mateke mwilini. 
 
Amesema mama huyo alifariki muda mchache kutokana na kupigwa sehemu 
mbalimbali za mwili wake na kusababishiwa majeraha makuibwa yaliyopeleka
 kupoteza uhai wake. 
Awali akizungumzia tukio hilo Mtoto wa Kwanza wa mama huyo Ndugu Razaro 
Mbwiga amesema kuwa mdogo wake alikuwa na tabia ya kugombana na mama 
yake marakwamara . 
Hata hivyo teyari mwili huo umekwisha chukuliwa hospitali na kuzikwa ambapo katika maziko hayo Chama cha Muungano wa kijamii (Mujata)
 umewataka vijana kujiepusha na vitendo viovu kama uvutaji bangi na 
pombe za kienyeji kwani ndio chanzo cha kutokea kwa vurugu nyingi. 
 
KWA HISANI YA  MBEYA BLOG | 
No comments:
Post a Comment