| 
Bi Arafa Issa Namaji(Pichani) mwenye 
umri wa miaka 39 mkazi wa kijiji cha Narung’ombe wilayani Ruangwa Mkoani
 Lindi  anaomba msaada wa haraka utakaomuwezesha kupata matibabu ya 
uvimbe ulio katika paji la uso uliotokana na maumivu makali ya kichwa 
baada ya kupata matibabu katika hospitali ya Ndanda na kuelekezwa kufika
 katika hospital yaTaifa ya Muhimbili(MNH) Kwa uchunguzi zaidi na matibabu.
 
  
Tatizo lilianza tangu mwezi february 
2012, alianza kwa kuumwa na kichwakwa maumivu makali sana na kipele 
kidogo kikatokea kwenye paji la uso, hivyo basi kadri kilipopungua 
maumivu ndipo kipele kiliendelea kuwa kikubwa hadi kuathiri macho na 
sehemu ya pua baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya Majirani na 
marafiki wa karibu walimshauri kwenda hospitali ya wilaya, alipofika 
Daktari  alimpa rufaa ya kwenda hopsitali ya Ndanda,hata hivyo Ndanda 
pia wakampa rufaa kwenda hospitali ya Taifa muhimbili kwa uchunguzi 
zaidi.kutokana na hali hali hiyo ngumu aliyonayo Kutokana na kuwa katika
 hali duni na hana mtu yeyote wa kumsaidia. 
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya 
Ruangwa wameichangishana kupata kiasi cha nauli pamoja na hela kidogo ya
 kujikimu kwa siku mbili, lakini bado anahitaji msaada zaidi wa pesa 
kwasababu atahitaji kuishi zaidi DSM Akiwa  katika hospital ya Muhimbili
 kwa ajili ya uchunguzi pamoja na matibabu yake Kwa alietayari kumsaidia
 anaweza kuwasiliana na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa 
wa Lindi,Abdulaziz Ahmeid kwa namba za simu0787176221 au 0756696048Kutoa ni Moyo ili kumsaidia mama huyu
 
 (Habari hii ni kwa Hisani ya Pwani Blog) | 
No comments:
Post a Comment