Pages


Photobucket

Saturday, November 24, 2012

ZIARA YA KINANA GEITA‏


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi leseni za wachimbaji wadogo machimbo ya Mugusu, Geita, katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo mkoani Geita. Jumla ya leseni 21 zilikabidhiwa kwa wachimbaji hao baada ya kutolewa na serikali ili kuwwezesha wachimbaji wadogo nao kunufaika na m,adini badala ya wachimbaji wakubwa tu.

 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizindua shina la wakereketwa wa CCM la wajasiriamali watengeneza fenicha katika mji mdogo wa Katoro mkoani Geita, jana. Nape aliwapa pia ,msaada wa sh. milioni moja kwa ajili ya wajasiriamali hao kukuza shughuli zao.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtuza msanii, Kasim Magembe, baada ya kuridhishwa na uhodari wake alipotumbuiza kwenye mkutano wa CCM uliofanyika uwanja wa Mpira, Geita leo

Nape Nnauye ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimiana na Machinga wa Katoro Geita

No comments:

Post a Comment