Na: Geofrey Nyang’oro
WATU wanne akiwamo mwanamke mmoja wanaodaiwa kuwavamia na kuwajeruhi mapadri wawili kwa risasi na nondo mkoani Iringa, wamekamatwa.
Watuhumiwa hao ambao ni wakazi wa Ismani 
wanahusishwa na matukio mawili ya ujambazi uliofanyika katika Parokia za
 Kanisa Katoliki lililopo eneo la Kihesa Iringa Mjini na Parokia ya 
Isimani iliyoko Iringa Vijijini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael 
Kamuhanda aliwaambia waandishi wa habari ofisni kwake jana kuwa 
watuhumiwa wote wamekamatwa kufuatia msako makli uliofanywa na polisi 
baada ya tukio hilo lililsababisha watu watatu kujeruhiwa.
Alisema nyumbani kwa mwanamke ndiko walikuta bunduki iliyotengenezwa kienyeji inayodaiwa ilitumika katika ujambazi huo.
Alisema nyumbani kwa mwanamke ndiko walikuta bunduki iliyotengenezwa kienyeji inayodaiwa ilitumika katika ujambazi huo.
“Upekuzi uliofanyika nyumba kwa nyumba katika 
nyumba ya mwanamke ikipatikana gobore iliyotumika kutekeleza uhalifu 
huo. Nyumba ya mtuhumiwa mwingine motto wa mwanamke huyo zilipatikana 
gorori 37 na gramu 100 za baruti,” alisema.
Katika matukio hayo watuhumiwa wanadiwa kupora Sh4
 milioni na Euro 100, huku wakiwashambulia kwa mapanga na risasi mapadri
 wawili, Padri Anjelo Burgio (66) wa Paroko wa Parukia ya Isamani na 
Msaidizi wake, Padri Herman Myala (36).
Mwingine aliyejeruhiwa kwenye matukio hayo ni Mlinzi wa Kanisa la Kiaskofu la Kihesa, Batholomeo Nzigiliwa.
Hali za majeruhi
Kamanda Kamuhanda alisema majeruhi wote wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa na kwamba mlinzi wa Kanisa la Kihesa Nzigilwa hali yake ikielezewa kuwa ni mbaya.
Alisema mapadri  Burgio na Myala, wote wanaendelea vizuri.
Kamanda huyo alisema kuwa wanaendelea kuwasaka watu wengine wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo.
Kamanda huyo alisema kuwa wanaendelea kuwasaka watu wengine wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo.
 
 


No comments:
Post a Comment