Pages


Photobucket

Tuesday, January 22, 2013

APOKEA KICHAPO BAADA YA KUKATAA KUTII AMRI NA KUWEKWA CHINI YA ULINZI WA POLISI


Kijana ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja jana alijikutana kwenye wakati mgumu baada ya kupokea kichapo kutoka kwa askari wa jeshi la polisi maeneo ya kigamboni mbele ya geti la Chuo Cha Mwl Nyerere mara baada ya Kukataa kutii amri ya polisi iliyomtaka kutulia na kufungwa pingu Mara baada ya askari hao kumkata na kumfunga pingu kijana huyo alijikuta akionyesha umwamba na kuwapima ubavu askari hao na kupelekea Kupokea kichapo hadi pale alipotiwa nguvuni na vijana hao wa Saidi Mwema.
 Mtuhumiwa ambaye kosa lake halikuweza kufahamika kwa haraka (katikatika) akipokea kichapo kutoka kwa askari polisi hao wawili mara baada ya kukataa amri iliyomtaka kutulia na kufungwa pingu
 Hapa mtuhumiwa alipogoma kupanda kwenye difenda ya Mwema na kupelekea Kupigwa tanganyika Jeki ilikupakizwa kwa nguvu
Wakazi wa kigamboni Waliojitokeza kuona pambano hilo kati ya vijana wa Mwema na Mtuhumiwa ambaye kosa lake halikufahamika mara moja ambalo liliteka hisia za wakazi hao wa Kigamboni

No comments:

Post a Comment