
Msanii/Muigizaji/Mchekeshaji Hussein Ramadhani Mtioeti (27) maarufu
SHARO MILIONEA
amefariki dunia katika ajali ya gari jijini Tanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Prudence Masawe, amethibitisha
kutokea kwa ajali na kusema kuwa marehemu amefikwa na umauti baada ya
gari lake aina ya  Toyota Haria lenye namba za usajili T478DVR kuacha njia na kupinduka.
Hili
 ni pigo jingine kwa Tasnia ya Filamu nchini Tanzania, hasa ukizingatia 
kuwa juma lililopita alifariki msanii Mlopelo na wakati Sharo Milionea 
anafariki tayari tasnia hiyo ya bongo Move ipo katika Msiba mwingine 
mzito wa Mcheza Filamu John Steven anaetarajiwa kuzikwa kesho.
Kamanda Massawe amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya
saa mbili usiku wa Novemba 26, 2012 katika kijiji cha Maguzoni Soga Wilaya ya
Muheza Mkoani Tanga.
Akisimulia
 zaidi RPC Massawe anasema kuwa marehemu alikuwa
akiendesha gari hilo na alikuwa peke yake bila abiria mwingine na ajali 
kumfika akiwa katika kijiji hicho kilichopo kati ya segera na Muheza.
“Marehemu ndie alikuwa akiendesha gari lile, na
lililopopinduka yeye alirushwa nje kupitia kioo cha mbele na umauti kumfika
hapo hapo” alisema Kamanda Massawe.
Aidha Kamanda Massawe amesema msanii huyo alikuwa akitokea jijini
Dar es Salaam na alikuwa akienda nyumbani kwao Muheza.
Inakumbukwa kuwa Msanii huyo aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa
staili yake ya utembeaji na uongeaji alipata Kunusurika katika ajali nyinge
mapema mwaka huu baada ya basi alilokuwa akisafiria la Taqwa kutoka nchi jirani
ya Burundi kupata ajali Mikese mjini Morogoro Januari 5 mwaka huu akirejea Dar
es Salaam.
 
MWEMA Blog inatoa salamu za Pole kwa Familia, wasanii
wa Filamu, Vichekesho na muziki nchini kwa Msiba huo mzito  hasa ukizingatia kuwa bado wapo katika Msiba
wa Mcheza filamu John Stephen anaetarajia kuzikwa kesho Makaburi ya Kinondoni. 
 
 

No comments:
Post a Comment