Pages


Photobucket

Sunday, November 25, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT GHARIB BILAL AWASILI MKOANI KATAVI NA KUZINDUA UWANJA NDEGE WA MPANDA NA KONGAMANO LA TATHMINI YA UWEKEZAJI UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Gharib Bilal na Mkewe mama Aisha Bilal wakishuka kwebye ndege mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi kwa ajili ya uzinduzi wa mkoa mpya wa Katavi unaofanyika mjini mpanda kesho, Makamu wa Rais pia amezinddua uwanja wa ndege wa Mpanda na kuzindua Kongamano la Tathimini ya Mkutano wa Uwekezaji Ukanda wa Ziwa Tanganyika uliofanyika Oktoba 17 mwaka jana na kushirikisha mikoa mitatu ya Rukwa, Kigoma a kufanyika mjini mpanda ambapo sasyamekuwa makao makuu ya Mkoa wa Katavi
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akisalimiana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda, kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe na katikati ni mama Tunu Pinda.
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal kushoto akijadiliana jambo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa Kongamano la kutathmini Mafanikio na Changamoto baada ya mkutano wa Uwekezaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika Kigoma na Rukwa uliofanyika Oktoba 17 mwaka jana mjini Mpanda
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza katika uzinduzi wa Uwanja wa ndege wa Mpanda, kshoto ni Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal na kulia ni mama Zakia Bilal.
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akizungumza wakati wa uzinduzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi leo mchana.
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar Chambo akitoa taarifa ya ujenzi wa uwanja huo kwa Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal wakati wa uzinduzi mjini mpanda leo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba akimkaribisha Makamu wa Rais ili kuongea na wananchi wakati wa uzinduzi wa uwanja huo mjini Mpanda leo
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kukamilika kwa ujenzi wa uwanja huo, kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda na Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba, kushoto ni Mama Zakia Bilal mke wa Makamu wa Rais.
Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye, Dkt. Mary Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Ofisi ya Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu na Mama Zakia Gharib Bilal Mke wa Makamu wa Rais wakiwa katika uzinduzi huoMakamu wa Rais akisalimiana na Mary Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwekezaji mara baada ya kuwasili mjini Mpanda leo Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Katavi Mselem na kutoka kulia ni Mbunge wa Mpanda mjini CHADEMA Mh.Said Arfi na Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt Charles Tizeba.
Makamu wa Rais Dkt Gharib Bilal akivishwa skafu na vijana wa chipukizi mjini Mpanda mara baada ya kuwasili mkoani Katavi leo.
Makamu wa Rais akisalimiana akipungia mkono wananchi waliofika kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi leo, kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe na kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa Bw. Mselem.
Makamu wa Rais Dkt Gharib Bilal na Mkewe Mama Zakia Bilal wakiangalia ngoma katika uwanja wa ndege wa Mpanda
Mama Tunu Pinda akishiki kuchza ngoma za asili za mkoa wa Katavi kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda wakati wa mapokezi ya Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal.
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akisalimiana na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba Bw. Nehemia Kyando Mchechu
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akifurahia jambo na Mzee Paul Kimiti Waziri Mkuu wa Zamani na Mbunge wa jimbo la Sumbawanga miaka iliyopita kwenye uwanja wa ndege wa Mapanda
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Mh. Venance Mwamoto wakati wa mapokezi hayo, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimpa ishara ya Dole Mbunge wa Mpanda mjini CHADEMA Mh. Said Arfi, wakati wa mazungumzo yao kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda katika mapokezi ya Makamu Wa Rais Dkt. Gharib Bilal, Kauli mbiu ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutegwe katika maendeleo mkoani Katavi inasema "SIASA NI MAENDELEO"
kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injini Stella Manyanya, Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Issa Machibya na mwenyekiti wa CCM Mpanda Hamida Mbogo wakizungumza mawili matatu wakati wa mapokezi ya makamu wa Rais mjini Mpanda leo,
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Mzee Chrisant Mzindakaya ambaye ni mwekezaji mkoani Rukwa na wwekezaji wengine kutoka India, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe akizungumza katika kongamano hilo kwenye ukumbi wa Idara ya maji mjini Mpanda na kukaribisha wageni mbalimbali waliohudhuria kongamano hilo.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injini Stella Manyanya akizungumza na kutoa taarifa ya mkoa wake katika suala zima la uwekezaji mkoani Kwake
Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Mary Nagu akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika mjini Mpanda leo
Mabalozi mbalimbali wamehudhuria katika sherehe hizo za uzinduzi wa mkoa wa Katavi kutoka Burundi, Zambia, Misri, Japan na DRC Kongo
Waziri katikati Charles Tizeba akiwa na viongozi mbalimbali wa Vyama, Serikali na Taaisisikadhaa wamehudhuria katika konamano hilo
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Issa Machibya akizungumza na kutoa taarifa ya mkoa wake katika suala zima la uwekezaji mkoani Kwake

No comments:

Post a Comment